Msasa Media

Msasa Media

By Msasa MediaNewsDaily News
Download on the App Store

Msasa Media episodes

  • KANYE WEST AJITOA KWENYE MBIO ZA KUGOMBEA URAIS WA MAREKANI.
    Wakati taifa la Tanzania likiwa kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2020, huku ikishuhudiwa muamko mkubwa wa wasanii na watu maarufu wakijitokeza kuchukua fomu kwaajili ya kuhitaji ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali. Nchini Marekani msanii Kanye West amejitoa kwenye mbio hizo za kugombea nafasi ya Urais.
    Rapa Kanye West alitangaza azma yake ya kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndani ya Marekani, huku akiwa anajaribu kushindana na Donald Trump ambae alikua ni rafiki yake kwenye harakati za kumsaidia kumfanyia kampeni wakati anataka kuingia White House.
    Taarifa za Kanye West kujiondoa kwenye mbio hizo zimetolewa na watu wa karibu sana ambao walikuwa kwenye kamati yake ya kampeni.
    Taarifa zinasema timu ya Kanye West tayari ilikuwa imeshaingia kwenye majimbo ya Florida na Carolina Kwaajili ya kuanza kuwaandaa baadhi ya wanahabari ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kampeni yao, jambo ambalo lilihitaji mawakili wengi kushiriki na kuliunga mkono.
    Kwenye taarifa hiyo, wanasema watu wengi walijitokeza kumuunga mkono rapa Kanye West na kusaini, namba ilikua kubwa mpaka ikatuzidi huku watu wengi waliamua sio tu kusimamia mikataba yao lakini walijitolea pia.
    Lakini baadae kidogo baada ya chanzo hicho kuulizwa kuhusu maendeleo ya timu ya kampeni ya Kanye, Jibu lilikua ni "Amejitoa" Pindi alipoulizwa zaidi kuhusu mwisho wa mbio za kugombea urais za Kanye West akajibu "Nitawafahamisha ninachojua mara moja"
    2 min
  • HUAWEI YAPIGWA MARUFUKU KUWEKA MITAMBO YA 5G NCHINI UINGEREZA.
    Uingereza imepiga marufuku Kampuni ya Huawei kuweka mitambo ya 5G huku kampuni kama BT (BTGOF) na Vodafone (VOD) zikipewa muda mpaka 2027 kuondoa mitambo ya kampuni hiyo kwenye mitandao yao.
    Waziri wa masuala ya kidigitali na Utamaduni, Oliver Dowden amesema kutokana na hali ya sintofahamu inayozunguka Kampuni hiyo ya china, Uingereza imekosa imani na mitambo ya 5G ya Huawei.
    Marufuku iliyotolewa na Uingereza ni ushindi mkubwa kwa Marekani ambayo imekua ikishinikiza Mataifa kupiga marufuku Kampuni hiyo kwa madai kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa.
    Uamuzi wa Uingereza umetejwa kuwa ni pigo kubwa sana kwa kampuni ya Huawei kwani soko muhimu kwa kampuni hiyo na 24% ya mauzo ya mwaka jana yalitokea huko.
    Vilevile Kampuni hiyo ya kichina ambayo imeanza kuzalisha bidhaa za mawasiliano tangu mwaka 1997 bado inaendelea kufanya vizuri sokoni kwa kuleta bidhaa mpya za simu na tablets.
    2 min
  • MENEJA WA DIAMOND, SALLAM SK ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA UNIVERSAL MUSIC GROUP AFRIKA MASHARIKI.
    Hayo yameelezwa na mwanamuziki Diamond Platinumz Wakati lebo ya WCB ikizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kuhusu usiku wa Zuchu utakaokuwa Julai 18 mwaka huu mlimani city jijini Dar es salaam.
    "Sijui kama nilitakiwa kusema hili au la, lakini bosi wangu Sallam atakuwa balozi wa Universal Music Group east Afrika (Afrika mashariki),na tunaamini kupitia yeye ataboresha zaidi", ametangaza Diamond.
    Mwanamuziki huyo amesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu uzoefu alioupata kwa kufanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka minne, na nini kinasababisha wasanii wengine kuilalamikia Kampuni hiyo.
    Akijibu amesema kuwa amejifunza mengi na kwa kiasi fulani amefanikiwa japo baadhi ya mambo hayakwenda kama alivyotarajia. Ameongezea kuwa uzoefu alioupata utamsaidia endapo ataingia mkataba tena na kampuni hiyo au kama msanii yeyote kutoka WCB ataingia mkataba,kwa sasa ataweza kuwashauri.
    Aidha amewashauri wasanii wenzake kwanza wajijengee mizizi ndani ya nchi kabla ya kufanya kazi na kampuni za nje kwani hizo hazina kujuana na pia wawe makini katika mikataba wanayoingia ili wasije wakaishia kupata hasara.
    2 min
  • MKE WA MSANII RAY J (PRINCESS LOVE), ASITISHA KUDAI TALAKA MAHAKAMA.
    Ule msemo wa wapendanao wakigombana chukua jembe ukalime, umeonekana kudhihirika baada ya Princess Love ambae ni mke wa msanii Ray J, kuamua kurudi mahakamani kusitisha kesi yake ya kudai talaka kutoka kwa mumewe.
    Princess Love alifungua file la kudai talaka mwanzoni mwa May, 2020 Baada ya kuwa Kwenye mahusiano ya ndoa na Ray J kwa kipindi cha miaka 4, huku wakifanikiwa kupata watoto wawili (Melody love & Epik Ray).
    Wawili hao wamekuwa hawaishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja sasa, huku sababu kubwa iliyopelekea kuachana ni kutokana na Ray J kusemekana kumuacha Princess Las Vegas wakati alipokuwa na ujauzito wa miezi 8 wa mtoto wao wa pili, Lakini ingawaje mpaka sasa bado haijafahamika sababu kubwa iliyopelekea Princess kusitisha kudai talaka.
    Kutokana na kurudi tena kwa mahusiano hayo, watu wa karibu wanadai kuwa hivi sasa wawili hao wamefanya hivyo ili kulea watoto wao ambao bado ni wadogo na wanahitaji malezi toka kwa wazazi.
    Kwenye moja ya mahojiano aliyofanya, Ray J amesema " Nina furaha sana kurudi tena kuishi pamoja na watoto wangu, tena ukizingatia wiki ijayo ni sherehe ya kuzaliwa ya mmoja kati ya watoto wangu, kwa kipindi chote cha Lockdown Nimekua nikijifungia studio tu.
    Ray J akaongezea kwa kusema, "mke wangu ni mama bora sana kwa watoto wake kwani naamini kila analofanya huwa na sababu.
    2 min
  • MJASIRIAMALI LAZIMA AELEWE MAMBO HAYA
    .Habari rafiki mpendwa, natumaini unaendelea vizuri na mapambano ya maisha.Nikutie tu moyo endelea na harakati hizo naamini ipo siku utayaona matunda ya unachokifanya.Kama kawaida leo nakuletea makala nyingine hii ni juu ya sifa za mjasiriamali.
    Kuna watu wengi sana wanajiita wajasiriamali lakini kiuhalisia si wajasiriamali.Hii imenifanya nifikirie juu ya hili.
    Zifuatazo ni sifa za mjasiriamali na kama huna sifa kati ya hizi basi hujawa mjasiriamali wa ukweli bali utakuwa unabip tu.
    sifa zenyewe ni kama zifuatazo,
    1. AWE NA MALENGO
    Hii ni sifa kubwa ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwa nayo, kwanza lazima uwe na malengo uliyojiwekea kwamba unataka kufikia wapi katika biashara yako.kama ni kuwa na pesa nyingi sema unataka kiasi gani kabla ya mwaka kuisha.kwa mfano; nataka kabla ya mwaka 2016 kuisha niwe nimetengeneza Milioni 20.Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii ili ufikie malengo hayo.
    2. AWE NI MTU ASIYE KATA TAMAA.
    Mjasiriamali yoyote duniani ni mtu ambaye si rahisi sana kukata tamaa katika kazi zake, watu wengi sana wamekuwa na malengo makubwa lakini wanashindwa kuyafikia kwasababu wanakata tamaa mapema sana,hii huwafanya warudi nyuma.Mfano mtu aliyeajiriwa anakuwa na malengo ya kujiajiri, anaanzisha biashara asipopata faida kama alivyotarajia hukata tamaa na kutamani tena kuajiriwa na hatimaye kutafuta ajira tena.Nikutie moyo tu hakuna kitu kinachokuja kwa urahisi kama unavyofikiria,kaza buti songa mbele changamoto ni chachu ya mafanikio.
    3. AWE NI MTU WA KUJIAMINI.
    Siku zote anayejiamini ndio hupata mafanikio kwa urahisi, watu wengi wamekuwa wakishindwa katika biashara zao kwa kushindwa kujiamini.Kumbuka hiyo ni biashara yako acha kuangalia watu wanasema nini wewe endelea tu na harakati zako ipo siku hao wanaokubeza watakusifia kwa unachokifanya.
    4. KUJALI MUDA WAKO.
    Muda ni kitu kidogo sana lakini muhimu kuliko kitu chochote, mbaya zaidi dakika moja au hata sekunde moja kupita hatokutana nayo tena katika mzunguko wa maisha yako yote.Kwahiyo kama umekuwa na malengo ya kufanya kitu fulani basi fanya haraka iwezekanavyo, ukizidi kuchelewa unaendelea kuweka matatizo na vikwazo katika kazi yako au hata biashara yako kuna msemo unasema"muda ni mali" au "time is money".
    Misemo hii imefananisha muda ni pesa, kwasababu pesa ni kitu muhimu lakini utapata pesa kwa kutumia muda vizuri.Acha kuahirisha mambo mara kwa mara fanya maamuzi sasa, kesho kamwe haitafika.
    5. AWE NA KAULI NZURI, TABASAMU NA NADHIFU.
    Hii ni nguzo muhimu sana kwa mjasiriamali, unapokuwa na kauli nzuri na mwenye tabasamu na nadhifu, unapokuwa unatoa huduma utawavutia wateja wengi zaidi na kama utakuwa na kauli mbaya na mchafu wateja watakimbia na mwisho wa siku unaanza kufikiria umelogwa kumbe wewe ndiye mchawi namba moja wa biashara yako. Zingatia hilo na utaona utakavyopata wateja kuliko kawaida.
    3 min
  • MBINU TANO ZA KUTAKA KUINGIA KATIKA BIASHARA.
    Zifuatazo ndizo hatua tano jinsi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio.
    1. Ainisha aina za biashara ambazo unataka kuzifanya.
    katika hili ni kwamba kama unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio, unatakiwa kuainisha aina mbalimbali za biashara ambazo unataka kuzifanya huwenda zikawa ni zaidi ya biashara hata sita.Ukisha pata biashara hizo jaribu kuwashirikisha hata baadhi ya ndugu na jamaa ili wakupe mtazamo wao ni biashara ipi inafaa.
    2. Chagua biashara moja ambayo unaona inafaa.
    Hatua ya pili baada ya kuwashirikisha ndugu na jamaa, unachotakiwa kufanya ni kwamba kaa chini pamoja na halmashauri yako ya kichwa ili kuweza kupambanua ni biashara ipi ambayo inafaa, baada ya kupata majibu tafakari kisha chagua mwenyewe biashara moja ambayo itakuwa na faida kwako hapo mbeleni.
    3. Fanya utafiti juu ya washindani wako.
    Baada ya kupata wazo moja la biashara hatua ya tatu ni kwamba unatakiwa kufanya utafiti wa juu ya washindani wako ambao tayari umewakuta wakifanya biashara.Na katika kufanya utafiti wako unatakiwa kujua ni mbinu zipi ambazo wao huzitumia katika kupata wateja, baada ya kujua hii itakusaidia kujua mbinu mpya ambayo itakufanya uweze kuwavuta baadhi ya wateja ili waje kwako.
    4. Tengeneza mpango wa biashara hiyo.
    Baada ya kujua mbinu za kuwatambua na kuwashinda washindani wako, jambo la nne ni kuhakikisha unaandaa mpango biashara ambao ndiyo utaongoza biashara yako.katika mpango wa biashara ndio ambao utakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua biashara yako jinsi ambavyo utakavyokuwa.Nakusihi tuu endelea kufuatana nami afisa mipango kila wakati nitakueleza siku nyingine jinsi ya kuandaa mpango wa biashara.
    5. Tafuta mtu atakaye kuongoza na kusimamia katika biashara yako.
    Mwisho kabisa ili uweze kufanikiwa katika biashara yako unahitaji kuwa na mtu wa kuongoza katika biashara yako, mtu huyo anatakiwa kuwa mzoefu katika biashara ambayo unatakiwa kufanya.Uzoefu w mtu huyo litakuwa darasa tosha kwako na kukuelekeza ni nini ufanye na nini usifanye.
    Lakini nikuibie siri moja, hatuna siri kubwa katika mafanikio makubwa ya kibiashara kama kuwa mbunifu, ubunifu ndio siri na silaha makini ya utendaji wako wa kibiashara yenye mafanikio.
    3 min
  • KAULI YA KWANZA YA SHILOLE TOKA APIGWE MUMEWE - UCHEBE
    Mwanamuziki wa bongo na mfanyabiashara Shilole ameibuka tena baada ya siku chache kuposti picha zikimuonyesha ameumizwa na mume wake baada ya kupigwa na mumewe leo ameibuka na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano Kipindi cha matatizo yake.
    Kupitia ukurasa wake wa instagram Shilole aliandika hivi
    Salaam ndugu zangu,
    Nimeona upendo, nimeona heshima na kukubalika kwa kiwango cha pekee katika wakati huu wa changamoto niliyokutana nayo.
    Nashukuru sana kwa upendo wenu, nashukuru sana wote walionijulia hali na kuniombea dua.
    Kuhusu maendeleo yangu mimi niko sawa naendelea kupambana.Changamoto ni sehemu ya maisha haziwezi kunifanya nianguke, lakini yote hayo si kwa nguvu zangu ni Mungu pamoja na watanzania wenzangu mnaonitakia mema.
    Maisha yanaendelea tuendelee kuijenga jamii yetu, jamii inayokataa unyanyasaji wa kijinsia.
    Kutokana na yaliyomkuta Shilole naamini kabisa bado katika jamii zetu mambo haya yapo na yanawakuta wanawake wengi hasa sehemu za vijijini kutokana na kwamba bado kuna mambo ya unyanyasaji wa kijinsia.
    Taarifa ya Shilole natumaini itakuwa imewagusa wengi ambao wanakutana na changamoto kama hizi na waweza kuamka na kuzipinga kwa kutoa taarifa sehemu husika ili wanaofanya vitendo hivi vya unyanyasaji wa kijinsia vifike kikomo na tuishi kwa amani katika jamii zetu.
    2 min
  • MWANAMKE WA KWANZA MWEUSI KUENDESHA NDEGE YA KIKOSI CHA WANAMAJI MAREKANI.
    Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.
    Ameandika historia kwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha "wings of Gold" au (mbawa za dhahabu), baadae mwezi huu wa Julai kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa alhamisi wiki hii na mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi za majini.
    Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi Swegle akitumia herufi"BZ" au "Bravo Zulu",neno linalotumiwa na wanajeshi wanamaji linalomaanisha"umefanya vyema".
    BZ kwa Lt.j.g Madeline Swegle kwa kumaliza Mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi ya mashambulio ya anga, aliandika mkuu wa mafunzo ya kijeshi ya ndege za kivita za majini.Swegle ni mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anaetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea mbawa za dhahabu baadae mwezi huu.
    HOOYAH!", Uliandikwa ujumbe wa mkuu huyo wa mafunzo.
    Kwa mujibu wa jeshi la majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kuhusu rubani huyu mpya Swegle kwasasa yuko katika kituo cha mafunzo cha Redhawks squadron (VT) 21 katika kituo cha ndege za vita vya majini-Naval Air station cha kingsville kilichopo Texas.
    2 min

About Msasa Media

From the publisher's feed

Msasaonline inaamini kila binadamu ana haki ya kuhabarika kuburudika, na kuelimika hivyo basi kazi yetu kuhakikisha tunakuletea habari sahihi, na kupunguza msongo wa mawazo kwa burudani nzuri na…