Msasa Media

Msasa Media

By Msasa MediaNewsDaily News
Download on the App Store

Msasa Media episodes

  • UHOLANZI: KUISHITAKI URUSI KATIKA MAHAKAMA YA ULAYA KWA KUIANGUSHA NDEGE YA MALAYSIA.
    Taifa la Uholanzi limesema litaishitaki Urusi katika mahakama ya Ulaya kuhusu haki za kibinadamu ya ECHR kwa hatua yake ya kuiangusha ndege ya shirika la ndege la Malaysia mwaka 2014.
    Jamaa wa wahanga 65 wa Uholanzi waliofariki kwenye ajali ya ndege waliwasilisha malalamiko yao kwenye mahakama hiyo yenye makao makuu mjini Strasbourg, wakiitaka Urusi kubeba dhamana ya tukio hilo ambapo watu wote waliokuwepo kwenye ajali hiyo walipoteza uhai.
    Uholanzi na Australia zimesema zinaibebesha jukumu kubwa nchi ya Urusi kwa kuiangusha ndege hiyo iliyokua safarini kuelekea Kuala Lumpur kutoka Amsterdan.
    Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi Stef Blok amesema upatikanaji wa haki kwa wahanga 298 wa ndege hiyo iliyokuwa na nambari za safiri MH17, utaendelea kuwa kipaumbele cha juu kabisa cha serikali yake.
    2 min
  • SYRIA: HOSPITALI ZAFUNGWA BAADA YA MGONJWA WA KWANZA WA CORONA KURIPOTIWA MKOANI IDLIB.
    Hospitali katika eneo la kaskazini magharibi mwa Syria zimeamua kusitisha huduma zisizokua za dharura baada ya kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya CORONA kuripotiwa.
    Vilevile idara inayosimamia elimu imetangaza kufunga shule zote. Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa afya, kisa cha kwanza cha Ugonjwa wa Covid-19 kiliripotiwa siku ya alhamisi ya tarehe 9, Julai 2020 katika mkoa wa Adlib, eneo la mwisho lililodhibitiwa na wapinzani.
    Daktari aliyegundulika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona tayari ameshajitenga na katika wadi maalumu ya hospitali ya Bab al-Hawa huku wagonjwa na wahudumu wengine wa afya aliokaribiana nao wakiwekwa Karantini.
    Kumekuwa na wasawasi mkubwa juu ya kuelemewa kwa mfumo wa afya katika eneo hilo la kaskazini magharibi mwa Syria lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 3.
    Vituo vingi vinavyotoa huduma za matibabu vimeharibiwa na vita vya muda mrefu nchini humo.
    Vilevile afisa wa shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt Michael Ryan amesema mifumo ya afya Duniani inahitajika kuendelezwa ili kudhibiti maambukizo ya magonjwa na kuweza kuwahudumia idadi kubwa ya wagonjwa katika wakati huu wa janga la Virusi vya Corona pamoja na majanga mengine yanayoweza kuzuka hapo baadae.
    2 min
  • MAREKANI YAIARIFU UN HATUA YA KUJIONDOA WHO.
    Serikali ya Marekani imeuarifu rasmi Umoja wa Mataifa juu ya uamuzi wake wa kujiondoa kutoka shirika la Afya Dunia (WHO), ifikapo mwaka 2021.
    Rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha taarifa hiyo siku ya Jumatatu kwa katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres. Mwishoni mwa mwezi Mei Trump alisema atajiondoa kwenye shirika hilo ikiwa ni katika kupinga namna inavyoshughulikia janga la Virusi vya Corona.
    Umoja wa Mataifa umethibitisha kupokea taarifa hiyo inayosema Marekani itajiondoa katika shirika hilo ifikapo Julai 6, 2021.
    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kulingana na nafasi aliyonayo Guterres kama mwenye dhamana ya katiba ya WHO ya mwaka 1949, yuko katika mchakato wa kuthibitisha ndani ya shirika hilo kama Marekani imetimiza masharti ya kujiondoa.
    Afisa mkuu wa Utawala wa Rais Trump aliiambia CBS NEWS kwamba Washington ilielezea mabadiliko inayohitaji WHO kufanya na kujadiliana nayo moja kwa moja, lakini shirika hilo limekataa kuchukua maamuzi.
    Taifa la Marekani limekua mwanachama wa Shirika la Afya (WHO) tangu Juni 21, 1948.
    4 min
  • KUELEKEA MCHEZO WA WATANI WA JADI (SIMBA NA YANGA), AZIM DEWJI ATOA NENO.
    Aliewahi kuwa mfadhili wa klabu ya Simba ya Kariakoo Jijini Dar es salaam, Tanzania "Azim Dewji ameliomba Shirikisho la mpira nchini Tanzania (TFF), kuupeleka mbele mchezo wa watani wa Jadi (Simba na Yanga) kwa Wiki moja zaidi ili kuupisha mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM ambapo utafanyika siku hiyo hiyo ya mchezo.
    Dewji ameyasema hayo wakati kukiendelea kwa matayarisho ya mchezo huo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho la TFF yakiendelea kufanyika kwa vilabu na mamlaka ya mpira.
    Mwanachama huyo wa klabu ya Simba amesema kuruhusu matukio hayo yote kufanyika kwa wakati mmoja, yatazuia wapenzi ambao ni viongozi katika chama cha CCM kushindwa kufuatilia mechi hiyo ambayo ina mvuto na inabeba tiketi ya ushiriki wa michuano ya kimataifa msimu ujao.
    Pia ameongezea kuwa katika mchezo wa watani wa Jadi uliopita, kiliendeshwa zoezi la uchangiaji wa damu na walioshiriki walizawadiwa fulana, lakini kwasasa watagawa jezi ili kuongeza chachu kwa mashabiki wa vilabu vyote viwili.
    Klabu ya Simba imeshafanikiwa kuuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, licha ya kubakiza michezo kadhaa ya kumalizia mojawapo ikiwa ni huo wa Jumapili hii dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    2 min
  • SHILOLE: ASIMULIA JINSI ANAVYOPIGWA SANA NA MUME WAKE "UCHEBE".
    Hatimae msanii Shilole kupitia ukurasa wake wa instagram, ameamua kuanika ukweli wote kuhusu ndoa yake na mumewe Uchebe jinsi unavyoendelea.
    Shilole amesema ni mara nyingi amekua akiambulia kipigo kutoka kwa Uchebe kwa sababu ambazo sio za msingi,
    Msanii ameongezea kwa kusema mume wake ni mara nyingi amekua akimuonesha upendo wa kweli na kumvumilia kwa mapungufu yake yote, huku akimpatia mali zake lakini hilo halikumfanya ashindwe kudharauliwa, kupigwa na kusalitiwa.
    4 min
  • RAIS WA BRAZIL "JAIR BOLSONARO" AMETHIBITISHA KUPATA CORONA.
    Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amethibitika kupata maambukizi ya virusi vya Corona, baada ya kuwa na tabia ya kupuuzia ugonjwa huo kwa kuuita mafua tu yasiyokuwa na athari kubwa.
    Taarifa ya maambukizi ilianza tangu siku ya Jumatatu baada ya kupimwa na kukutwa na kiwango cha juu cha joto.
    Aidha Jair Bolsonaro pia alikua amewataka magavana kulegeza masharti yaliyowekwa kama njia moja ya kukabiliana na Ugonjwa wa virusi vya Corona akisema kuwa hatua hizo zimeathiri uchumu, huku yeye mwenyewe siku hiyo ya Jumatatu akisahau kuvaa Barakoa.
    Rais huyo wa Brazil alishawahi kusema kuwa hata kama akipata Corona, hatakuwa na wasiwasi wowote sababu zaidi itakua ni kama mafua tu au homa.
    Alipokua anatoa hilo tangazo, idadi ya waliothibitika kupoteza uhai kutokana na maambukizi ya Covid-19 ilikua bado ni chini ya 3,000 huku maambukizi yakiwa ni 40,000, lakini idadi imekua ikiongezeka tangu wakati huo.
    Lakini licha ya idadi kuzidi kuongezeka Rais Bolsonaro amekua akisema kuwa athari za kufungwa kwa maeneo ni kubwa sana kuliko za virusi vyenyewe, na kuvishutumu vyombo vya habari kwa kusababisha hofu kwa raia wake.
    Mpaka sasa idadi ya waliofariki nchini Brazil imeshafikia 66,868 huku waliopona wakiwa ni milioni 1.7 na waliothibitika kuwa na maambukizi ni milioni 1.67, lakini Taifa la Marekani likiwa linaongoza kwa kuwa na maambukizi Milioni 3.5, waliopona ni 918,000 na waliofariki ni 133,000.
    2 min
  • INDIA: UUZAJI WA NYAMA YA MBWA YAPIGWA MARUFUKU.
    Mkoa wa Nagaland unaopatika mashariki mwa India imepiga marufuku uuzaji wa nyama ya mbwa iliyokua inafanyika kwa muda mrefu.
    Kulingana na taarifa iliyotolewa na jarida la The Indian Express, ni kwamba katibu wa jimbo la Temjen Toy nchini India amesema kwamba Serikali yake imechukua uamuzi wa kupiga marufuku biashara ya kuuza nyama ya mbwa kwa hali yoyote.
    Siku zote nyama ya mbwa imekua ikiliwa kitamaduni katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa India.
    Baadhi ya mashirika ya kiraia katika maeneo hayo yamekemea uamuzi huo wakati ambapo shirika la kimataifa la haki za wanyama limepongeza uamuzi huo uliochukuliwa na serikali.
    Zaidi ya mbwa 30,000 kila mwaka huuzwa katika masoko ya majimbo hayo ambayo yana utamaduni wa kula mbwa kaskazini mashariki.
    8 min
  • HISPANIA: YATANGAZA HATUA MPYA ZA KUZUIA COVID-19 KUSAMBAA.
    Jimbo la Galicia lililoko kaskazini magharibi mwa Uhispania limeweka hatua mpya za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona kutokana na mlipuko mpya wa Virusi hivyo.
    Uamuzi huo umechukuliwa siku moja baada ya jimbo la Catalonia kutangaza masharti yanayowazuia watu kutoka nje ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.
    Aidha serikali ya India imeamua kutolifungua tena eneo la kihistoria la Taj Mahal, kutokana na maambukizi kuongezeka kwa kasi kwenye mji wa Agra.
    Naye Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amefuta maadhimisho ya uhuru wa nchi hiyo pamoja na sherehe za kuapishwa kwake kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19.
    Mexico jana imerekodi maambukizi mapya 4,683 ya virusi vya Corona pamoja na vifo 273.
    Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn ameonya kwamba Virusi vya Corona bado vipo, hivyo ni muhimu kuendelea kuvaa barakoa kila siku.
    Vilevile Rais wa Madagascar alitangaza dawa ya kunywa ya miti shamba inayotokana na mmea wa pakanga pamoja na mimea mingine inayoweza kutibu maambukizi ya virusi vya Corona.
    Madagascar imekuwekea mji wake mkuu Antananarivo amri ya kutotoka nje kufuatia ongezeko jipya la maambukizi ya virusi vya Corona,Miezi miwili baada ya masharti hayo kuondolewa , ametangaza rais.
    Katika taarifa, eneo la Analamanga ambalo ndilo lenye mji mkuu linafungwa tena, rais alisema.
    "Hakuna magari yatakayoruhusiwa kuingia ama kutoka katika eneo hilo kuanzia leo Jumatatu hadi Julai 20 na masharti makali yatawekwa kwa wanaotoka".
    2 min
  • MADHARA YA KUKAA NA MKOJO KWA MUDA MREFU.
    Utakubaliana na mimi kwamba kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiari kwamba sasa mtu anaamua ngoja sasa nibanwe na mkojo,hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda,au vinywaji tunavyotumia.Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature's call.
    Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini,akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, Mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kupunguza maji hayo kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza wito huu wa asili.Mambo haya tunayafanya sana utasikia mkojo umebana kweli ila ngoja nimalizie hii kazi alafu nitaenda kujisaidia hivi ndiyo watu wengi wanafanya.
    Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo mkojo unapofika karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa.Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili RECEPTORS vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, Baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.
    Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani,automatic kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwakuwa Ubongo nao hutuma taarifa kwenye kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo utashindwa kufanya kazi ya kutoa taarifa au uwezo wa ubongo kuwa mdogo,Na matokeo yake itakuwa huwezi tena kuvumilia hata kwa muda ulio mdogo na utajikuta unajikuta umeshalowanisha nguo.
    Madhara mengine ni kwamba mtu akibana sana mkojo kwa muda mrefu na mkojo ukashindwa kutoka kwa wakati basi ni wazi kupata magonjwa kama U.T.I na pia utasababisha ugonjwa wa kibofu(bladder infection), Magonjwa ya figo na machafuko wa damu, bacteremia.
    Mpenzi msomaji ni vyema tukawa wasikivu pale mtu anapobanwa na mkojo,hii ni kwaajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwaajili ya afya yako kwa ujumla, kama unalo tatizo usisite kuonana na wataalamu wa afya.
    3 min

About Msasa Media

From the publisher's feed

Msasaonline inaamini kila binadamu ana haki ya kuhabarika kuburudika, na kuelimika hivyo basi kazi yetu kuhakikisha tunakuletea habari sahihi, na kupunguza msongo wa mawazo kwa burudani nzuri na…