
Sign up to save your podcasts
Or


Moja ya taarifa iliyoshangaza ulimwengu wa burudani jana, ilikua ni baada ya Msanii wa RnB "August Alsina" kusema kuwa ni miaka minne sasa amekua kwenye mahusiano ya kimapenzi na mke wa Will Smith, Jada Pinkett Smith japokua ilikua ni siri lakini alipata baraka zote kutoka kwa Will.
Sasa baada ya taarifa hiyo kufikia watu mbalimbali, kumekua na mapokeo ya kitofauti kwani wengi wao wanasema wala hawaendani kuwa wapenzi japo umri sio ishu kubwa.
Lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa baada ya Alsina kuweka wazi, mwana mama Jada Pinkett Smith pamoja na mume wake wamejitokeza kila mmoja kwa wakati wake na kukana taarifa hizo, kwa kusema hayo maneno ya August Alsina hayana ukweli wowote.
Will Smith na Jada Pinkett Smith Kwasasa mahusiano yao ni ya ushirikiano (Partnership) na ni kwa muda mrefu hawashiriki tendo la ndoa, na kutokana na makubaliano yao kila mmoja anaweza kufanya jambo lolote bila kipingamizi.
Mbali na August Alsina kuwa na miaka 27, huku Jada kuwa na miaka 48, Mahusiano ya ndoa ya Jada Pinkett Smith na Will Smith mpaka sasa yana umri wa miaka 23.
From the publisher's feed