Msasa Media

Msasa Media

By Msasa MediaNewsDaily News
Download on the App Store

Msasa Media episodes

  • SOMALIA: MWANDISHI AFUNGWA MIEZI 6 KWA KUIKOSOA SERIKALI KUHUSU CORONA.
    Mahakama ya Somalia imemuhukumu mwandishi wa habari maarufu nchini humo, Abdiaziz Ahmed Gurbiye kifungo cha miezi 6.
    Abdiaziz ambae ni mhariri mkuu na naibu mkurugenzi wa shirika binafsi la Goobjoog, mjini Mogadishu, alishtakiwa kwa kuikosoa Serikali ya Somalia katika kukabiliana na mlipuko wa Corona.
    Mahakama ya mjini Banadir ilimtaka kutoa faini ya shilingi milioni 5 za Somalia (208.3 USD) kwa kuchapisha taarifa za kizushi na kuitusi Serikali na mahakama, muda mfupi baada ya kuhamishiwa katika Gereza la Mogadishu.
    Wakili wake anasema Mahakama ilitumia sheria iliyopitwa wakati wa kutoa hukumu hiyo.
    Kesi ya Gurbiye imekua ikiendelea kwa miezi kadhaa, ilikua ni miongoni mwa kesi kubwa dhidi ya waandishi nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni.
    2 min
  • RWANDA NA BURUNDI: ZATANGAZA SIKU 3 YA MAOMBOLEZO KUTOKANA NA KIFO CHA MKAPA.
    Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia July 27 - 29, 2020 kufuatia kifo cha aliekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.
    Kagame ambae pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) amemzungumzia Hayati Benjamin kama kiongozi ambae mchango wake ulienda nje ya mipaka ya Tanzania.
    Vilevile Serikali ya Burundi imetangaza siku 3 za maombolezo kutokana na kifo cha Benjamin William Mkapa.
    Waziri mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni atakaeiwakilisha nchi yake katika msiba huo, ameshawasili jana nchini Tanzania na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Kigoma, CP Thobias Andengenye katika mpaka wa Manyovu.
    Rwanda na Burundi zinaungana na Watanzania kuomboleza kifo hicho na bendera za nchi hizo pamoja na ile ya Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) zitapepea nusu mlingoti.
    2 min
  • VIONGOZI WA AFRIKA WASHINDWA KUPATANISHA MZOZO WA MALI.
    Viongozi wa Mataifa ya Afrika magharibi wamemaliza siku nzima wa mkutano wa kilele hapo tarehe 24, Julai bila ya kufukia makubaliano juu ya mgogoro wa kisiasa unaotokota nchini Mali.
    Viongozi watano wa Mataifa ya Afrika magharibi wamekutana na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, pamoja na viongozi wa vuguvugu la maandamo wanaomtaka ajiuzulu.
    Hata hivyo, upatanishi ilishindikana,na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou pamoja na wenzake wa Senegal,Ivory Coast, Ghana, Nigeria wamesema jumuiya ya uchumi wa Mataifa ya Afrika magharibi, ECOWAS itaitisha mkutano mwingine wa kilele Jumatatu.
    Vuguvugu la Juni 5 lililopewa jina la siku yalipoanza maandamo hayo,linamtaka Keita aondoke madarakani kwa kushindwa kushughulikia uliyoporomoka nchini humo ufisadi pamoja na uasi wa miaka minne wa makundi ya kijihadi.
    2 min
  • CHINA YAIAMURU MAREKANI KUFUNGA OFISI YAKE YA KIDIPLOMASIA CHENGDU.
    Wizara ya mambo ya nje ya China,imeiamuru Marekani kufunga jengo lake la kidiplomasia lililopo Chengdu China, Uamuzi umekuja baada ya Marekani kufunga ofisi ya kidiplomasia ya China iliyopo Texas, Marekani.
    Kufungiana ofisi za kidiplomasia linaonekana kuwa suala linalozidi kuleta utengano kwa Mataifa hayo ambayo awali yalianza kwa kuwekeana vikwazo katika upatikanaji wa VISA,na kuongeza sheria kwa wanaosafiri kidiplomasia.
    Awali, Marekani ililaumu ofisi za China wanasaidia wizi wa kijeshi unaoiba tafiti za wamarekani.pia, walilaumu watu wa ofisi hizo kutumia majina yasiyo halisi katika kufanikisha suala la kuiba taarifa za kiintelijensia.
    Maafisa wa China wanasema utawala wa Rais Trump unaonyesha chuki ya wazi kwa wachina na wamelaumu Pompeo kwa kuendeleza itikadi ya vita baridi.
    Vile vile China imemkosoa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, akimtuhumu kusambaza uongo wa kisiasa kuhusu China.
    Pompeo aliishutumu China kwa kuendesha kambi ya watu wengi katika jimbo la magharibi la Xinjiang, na wizi wa taarifa za kitaaluma na siri za kibiashara.
    Wang aliwashutumu wanasiasa wa sasa wa Marekani kwa kuchochea makusudi kile alichokiita "Mabishano ya kiitikadi" kati ya nchi hizo mbili, ili kubadili mkondo wa mtazamo wa raia wa Marekani.
    2 min
  • WATU ZAIDI YA MILIONI 1.8 WANATAFUTA HIFADHI NCHINI UJERUMANI.
    Idadi ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Ujerumani kutokutoka na vita ama mateso katika nchi zao iliongezeka kupita milioni 1.8 mwishoni mwa mwaka jana kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa tarehe 23, Julai.
    Idara ya takwimu ya serikali kuu (Destatis) imesema kuwa nb idadi hiyo iliongezeka kwa kiwango cha chini cha kila mwaka kutoka asilimia 3 mnamo mwaka 2012, idadi hiyo ilijumuisha raia wa kigeni ambao walikuja nchini Ujerumani kwasababu za kisheria, kisiasa ama kibinadamu.
    Mnamo Desemba 31, takribani watu 266000 miongoni mwa waomba hifadhi hao walikuwa bado wanasubiri uamuzi wa mwisho wa maombi yao ya kutafuta hifadhi, idara hiyo ya (Destatis) imeripoti kuwa kiwango hicho ni asilimia 13 chini ya kile kilichoshuhudiwa wakati sawa na huo wa mwaka jana.
    Hii inahusishwa na ufanisi uliopatikana katika kazi iliyoko pamoja na kupunguzwa kwa ujumla wa kiwango cha maombi ya kutafuta hifadhi.
    2 min
  • LIBYA: MIILI YA WATU 7 WAGUNDULIWA KATIKA KABURI LA PAMOJA.
    Miili ya watu 7 imegunduliwa katika kaburi moja katika mji uliokuwa umetekwa na waasi Libya.
    Miili ya watu 7 ambao wanakisiwa kuwa raia imegunduliwa katika mji wa Terhune, mji ambao ulikuwa umetekwa na waasi nchini Libya.
    Mji huo ulikombolewa mnamo June 5 baada ya makubaliano makali kati ya jeshi la serikali inayotambulika na jumuiya ya kimataifa na wapiganaji wa jenerali Khalifa Haftar.
    Kiongozi wa jopo lililoandaliwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu mauaji katika maeneo yaliyokuwa yametekwa na waasi Libya Kemal es Seyewi amefahamisha kuwa
    katika hatua iliyopigwa hadi kufikia sasa ni miili ya watu 7 ndio iliyogunduliwa katika kaburi la pamoja.
    Miili hiyo imepelekwa katika hospitali moja uhifadhiwe na kuzikwa kwa heshima.
    Kulingana na taarifa zilizotolewa na serikali hiyo inayotambulika na jumuiya ya kimataifa, Terhune kuna zaidi ya makaburi 11 ya pamoja.
    Wapiganaji wa Haftar waliondoka katika eneo hilo baada ya kuzidiwa na mashambulizi yaliyoendeshwa kwa ushirikiano wa jeshi la Uturuki.
    2 min
  • JAJI MKUU WA IRAN AMESEMA HAWATIKISWI NA VILIO KUHUSU ADHABU YA KIFO KWA WAANDAMANAJI.
    Jaji mkuu wa Iran Ebrahim Rais amefifisha matumaini kwamba adhabu ya kifo iliyotolewa kwa waandamanaji watatu vijana wa kiiran itafutwa kufuatia malalamiko ya mitandaoni.
    Jaji mkuu huyo amesema maandamano yanakubalika lakini machafuko na fujo vinavyohatarisha usalama wa taifa ni mstari mwekundu.
    Ameongeza katika matamshi yaliyochapishwa na shirika la habari Isna, kwamba katika matukio kama hayo mahakama haiwezi kushawishiwa na kampeni na propaganda.
    Chini ya hashtag ya kupinga hukumu hiyo ya No ToExecution, mamillioni ya raia wa Iran wametumia Mitandao ya kijamii kupinga hukumu baada ya mahakama ya juu kuthibitisha adhabu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Amirhossein M, Mohammad R, na Saeed T.
    Msemaji wa wizara ya sheria ya Iran Gholam Hussein Ismail amesema wanaume hao waliongoza magenge ya vurugu na walijirekodi video wakichoma moto majengo kadha na miundombinu ya usafiri wakati wa maandamano ya Novemba, mwaka 2019.
    Novemba mwaka jana,Iran ilitikiswa na maandamano ya siku kadhaa yaliyochochewa na kupanda kwa bei ya mafuta. Hata hivyo, maandamano hayo yalizimwa na vikosi vya usalama.
    2 min
  • HUMAN RIGHTS WATCH YAIKOSOA JAPAN KWA UDHALILISHAJI WATOTO KATIKA MAANDALIZI YA OLIMPIKI.
    Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch,limedai kuwa kuna Utamaduni wa udhalilishaji wa kimwili wa kimaneno unaowalenga wanariadha vijana nchini Japan,Ikiwa imesalia mwaka mmoja kuelekea mashindano ya michezo ya olimpiki ya dunia yanayopangwa kufanyika mjini Tokyo.
    Shirika hilo limesema lilifanya mahojiano zaidi ya 50 na wanariadha watoto wa sasa na wa zamani kwa ngazi tofauti za mashindano, utafiti wa mtandaoni na mashirika ya michezo.
    Waligundua kuwa watoto nchini Japan,bado wanapitia udhalilishaji michezoni na limeainisha maswala ya kitaasisi ambayo yanayofanya uitikiaji wa taifa hilo kwa matukio kama hayo kukosa ufanisi.
    Shirika la michezo la Japan limesema linafahamu Kuhusu ripoti hiyo na kuongezea kuwa limechukua hatua kuondoa udhalilishaji kwenye michezo, ikiwa ni pamoja na kuunda Mtaala wa mafunzo au kutengeneza miongozo kwa mashule.
    2 min
  • FAIDA ZA KUTUMIA MITANDAONI YA KIJAMII ILI KUTANGAZA BIASHARA YAKO.
    1. Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako.
    Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana katika mitandao ya kijamii hivyo kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla.
    2. Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka.
    Kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yako kuna kuongezea wigo wa wateja wapya ambao ni vigumu kufahamu kuhusu biashara yako kwani wako mbali na eneo la biashara husika lakini Mitandaoni ya kijamii inakupatia nafasi ya watu wote watakao Kutana na tangazo la biashara yako kuifahamu na kushawishika kutumia bidhaa zako na hivyo kugeuka wateja wa biashara yako.
    3. Inajenga uhusiano wa karibu na wateja wako.
    Kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara yako na wateja wako hii inasaidia kuweka ukaribu wa kusikiliza maoni, shida na kutafuta ufumbuzi kiurahisi wa kero za wateja wako kwani kwa urahisi kabisa wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia akaunti za biashara yako za mitandao ya kijamii.
    4. Inaongeza imani na uaminifu wa watu kwenye biashara yako.
    Moja ya malengo ya kila biashara ni kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa bidhaa za biashara hiyo, hivyo Mitandaoni ya kijamii kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara na wateja wake na urahisi wa taarifa za biashara yako kumfikia mteja inapeleka kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa biashara yako.
    5. Inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako.
    Biashara nyingi hutumia fedha nyingi kwaajili ya kujitangaza na hili huonekana pale ambapo njia zinazotumika kutangaza biashara husika zinakuwa ni ghali sana na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara husika. Kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza inapunguza gharama hizo na kujitangaza na kupelekea kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara na kuipatia nafasi nzuri ya kifedha zaidi.
    6. Inaongeza ufahamu wa kutosha dhidi ya soko husika na wateja wako.
    Kupitia ukaribu unaojengeka wateja wako katika mitandao ya kijamii na kujibu comments za wateja wako katika mitandao ya kijamii hii inapelekea biashara husika kupata taarifa za kutosha za soko husika na kuipa nafasi biashara kuwa na taarifa za kutosha za wateja wake na hii inasaidia biashara Kufanya maamuzi na kuweka mikakati inayohitajika kwa wakati husika na soko husika.
    Hizo ni baadhi ya faida za kuitumia mitandao ya kijamii kuitangaza biashara yako na kama bado haujaanza kutumia mitandao ya kijamii ni vyema ukaanza sasa kwani unapitwa na mengi ambayo biashara yako ingenufaika kwa kutumia mitandao ya kijamii.
    Asilimia 90 ya wataalamu wa masoko wanakiri kuwa Mitandaoni ya kijamii ina nguvu sana katika kutangaza biashara na imekuwa ikionyesha matokeo chanya katika biashara zao.baadhi ya mitandao ya kijamii inayotumika sana katika matangazo ya biashara ni kama Facebook, Instagram, Twitter, Blogs, YouTube, LinkedIn,nk.
    4 min
  • MBINU MPYA ZA KUMFANYA MTEJA WAKO KUWA MFALME.
    Naomba pasipo kupoteza wakati nikukaribishe katika somo letu la leo,na siku ya leo tutazungumza kuhusiana na mbinu moja itakayo kusaidia katika ukuaji wa biashara.
    Moja kati ya changamoto kubwa kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea, nasema hivi kwasababu wafanyabishara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja ni mfalme, lakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao huona ufalme huo.
    Hii ni kwasababu wafanyabishara wachache sana ambao wamekuwa wakijua ni nini maana ya mteja.
    Wafanyabishara wengi wamekuwa wakimchukulia mteja pale anapokuja kwenye biashara ambayo anafanya tu.kufanya hivi kutakufanyanya kuiona ramani ya biashara haina usawa kwani biashara utazidi kuiona ni ngumu siku zote.
    Hivyo ili uweze kumfanya mteja wako awe mfalme unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;
    1. Acha mara moja kumsubiri mteja wako aje kukufuata mfanyabiashara mahali ulipo, bali anza utaratibu wa kumfuata mteja wako mahali alipo, Kufanya hivyo kutamfanya mteja wako ajisikie huru na pia ajihisi kuwa yeye ni mfalme kweli na kufanya hivi kutamjengea utaratibu mpya na pia kujiona yeye si kama tu mteja bali ni sehemu ya biashara yako.
    2. Tengeneza utaratibu mpya wa kuwa na mawasiliano ya karibu na mteja wako,si umekuwa ukisema ya kwamba mteja ni mfalme, kama ndivyo hivyo basi hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano na wateja, Mawasiliano hayo basi naomba yawe ni kwaajili ya biashara tuu na si vinginevyo na kama ukiyatumia mawasilaino hayo vibaya basi jiandae kuwapoteza wateja wako wote, Mawasiliano hayo yanatumika kuwajuza wateja wako kuhusu ujio wa bidhaa mpya na mambo mengine muhimu kuhusu biashara tu.
    3. Jifunze mbinu mpya ya kuweza kufanya mazungumzo na wateja, hivi hujawahi enda katika biashara ya mtu mwingine mpaka ukajuta kwanini ulienda mahali hapo, bila shaka kama hali hii imewahi kukutokea basi ni vyema katika biashara yako uweze kujenga utaratibu mpya ambao utakufanya wateja wako wajisikie huru kila wakija kwako.
    4. Uchawi mkubwa ambao unafanyika katika biashara ni kutoa ofa kwa wateja wako.
    Hii siri ambayo nakuibia wewe siku ya leo, haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya ila ili uweze kukua katika biashara hiyo ni vyema ukajiwekea utaratibu wa kutoa ofa kama yafanyavyo makampuni ya simu Kufanya hivyo kutawafanya wateja wengi waje kwako.
    Asante sana kwa kusoma makala haya, mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie kazi njema na siku njema.
    3 min

About Msasa Media

From the publisher's feed

Msasaonline inaamini kila binadamu ana haki ya kuhabarika kuburudika, na kuelimika hivyo basi kazi yetu kuhakikisha tunakuletea habari sahihi, na kupunguza msongo wa mawazo kwa burudani nzuri na…