Maji yamekupwa, fukwe tonge tonge, zimerowana
Mapande ya mafupa, sasa juu kweupeni, twayaona
Ya watu walotupwa, mkondoni, chombo chao kilipozama
Mifupa mipevu mizito, ya wanaume na kinamama
Mifupa michanga ya kitoto, ya vijana na wasichana
Umma ulipoghariki
Kwenye Bahari ya Kati
Wakikimbia hilaki
Na mateso Afrika
Mauaji Arabuni
Na mauti ya Asia
Wengine watarazaki, dhana raha za Ulaya!