Karibu kusikiliza Makala ya Nitunze Nikutunze.
Makala hii huruka kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 1 na Nusu Usiku kupitia Pangani FM ikiwa kwa lengo la kujadili Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi na kutafuta njia mbadala ya kukabiliana nayo pamoja na njia salama ya kuhifadhi taka na kutunza mazingira kwa Maendeleo Endelevu.
Episode hii ya Nitunze Nikutunze inaangazia juu ya swala Zima la kulinda Tabaka la Ozoni kwa ustawi wa mazingira na Viumbe Hai.
Katika jitihada za kuhifadhi tabaka la ozoni mwaka 1996 Serikali ya Tanzania iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong'onyoa tabaka la ozoni nchini.
Kama sehemu ya jumuiya ya kimataifa hadi sasa Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86 ya kiasi cha matumizi ya kemikali zinazomong'onyoa tabaka la ozoni.
katika jitihada za kuhifadhi Tabaka la Ozoni, mwaka 1996, Serikali ya Tanzania iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa tabaka la ozoni ili kuhakikisha kwamba hakuna sekta ya uchumi au jamii inaathirika kutokana na matakwa ya Itifaki ya Montreal. Aidha, programu hii ilianzisha utaratibu wa kusimamia na kudhibiti uingizaji wa kemikali na bidhaa zenye kemikali zinazoharibu tabaka la Ozoni kutoka nje ya nchi.
kipindi hiki kimejadili maana ya Tabaka Ozoni, athari zake na namna ambavyo linamhusu kila mtu katika maisha yake ya kila siku na jukumu la Jamii katika kutunza Tabaka Ozoni.
Ndani ya Kipindi hiki utamsikia Afisa mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muuungano na Mazingira nchini Tanzania Pamoja na sehemu ya Hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene katika Maadhimisho ya katika Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni,Maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dodoma siku ya Tarehe 17 mwezi Septemba mwaka 2020.