Karibu usikilize Makala maalumu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani katika Kipindi cha Jinsia na Maendeleo, ambacho hukujia mubashara kila siku ya Ijumaa Saa 10:30 jioni na kurudiwa siku ya Jumamosi Saa 2:30 asubuhi.
Katika makala haya maalumu, Rais wa Radio Maria Tanzania ndugu Humphrey Julius Kira, ameeleza kwa undani namna Taasisi hii ilivyotekeleza kwa vitendo Sera ya usawa wa Kijinsia, hali kadhalika pongezi za Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) Dakta Rose Reuben kwa ilichofanya Radio Maria Tanzania.