Msikilizaji karibu uungane na Shemasi Benedict Paschal Ndinde, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustini Peramiho Jimbo Kuu Songea, kwenye kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, ambapo anajibu swali la msikilizaji wetu kutoka Parokia ya Peramiho Jimbo Kuu la Songea , aliyeuliza “Kwa nini wakatoliki hatunywi Damu ya Kristo wala kuchovya wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu?”