Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Huku Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Na kwamujibu wa uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari bingwa kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 ulibaini asilimia 79 ya watanzania wazee waligundulika kuugua magonjwa ya kisukari.Basi kupitia kipindi chetu cha Siha Njema kwa mara nyingine kwa juma hili nitaweza angazia juu ya Ugonjwa huu na naama ya kukabiliana na ugonjwa huu.