Wakati dunia ikiadhimisha, siku ya kuhamasisha raia wa nchi tofuati kuhusu namna ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria Aprili 25, Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani, WHO ripoti,,iliyongazia mwaka mmoja uliopita,mikakati iliyowekwa kuzuia ,kupima na kutibu Malaria ziliathirika katika thuluthi tatu za mataifa ya ulimwengu , kutokana na janga la Corona.
Katika Makala ya Siha Njema tunaangazia juhudi tofuati za kupambana na Malaria barani Afrika ikiwemo majaribio ya chanjo ya Malaria nchini Kenya,Ghana na Malawi.