KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI
Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande mbili tofauti.
Kama tuna upendo kwa MUNGU inatupasa sana kushirikiana na MUNGU na kuwasiliana na MUNGU Mara kwa Mara.
Mawasiliano hayo ni maombi . Lakini maombi tu hayawezi kuzaa matunda kama sio maombi ya imani.
Kama kuna mambo matano(5) muhimu katika maombi yako basi ni hivi:
=Jina la YESU KRISTO(Yohana 14:14),
=Damu ya YESU KRISTO(Ufunuo 12:11),
= Neno la MUNGU la ufunuo wa ROHO MTAKATIFU(Zaburi 107:20),
=Nguvu za ROHO MTAKATIFU(Luka 1:35a)
=Na Kuomba kwa imani(Waebrania 11:6)