Tumeshuhudia mambo mengi sana katika ligi kuu Tanzania bara lakini sisi SportsCast tumeamua kukuletea uchambuzi wa mbinu zilizotawala katika msimu huu.
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu mbalimbali za makocha wa vilabu vya soka katika ligi kuu.
Tumeangazia ubora wa wachezaji katika kila nafasi tukianza na magoli kipa hadi washambuliaji wa kati.
Tumegusia namna timu mbalimbal zinavyoanza mashambulizi kutokea nyuma kupitia kwa mabeki wao wa kati na mapungufu ya namna hiyo ya kuanzisha mashambulizi.
Ubora wa Clatous Chama nao hatujaufumbia macho kwani tumechambua mchango wake katika safu ya kiungo ya Simba na namna timu nyingine zinavyotamani kuwa na kiungo kama yeye.
Tumeongelea kwanini mfumo wa 4-2-3-1 umetumika sana katika ligi kuu msimu huu huku tukiangazia kwa undani timu zilizotumia mfumo huo.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse:
https://www.clubhouse.com/club/sportscast