Shirika la afya duniani, limeiorodhesha Kenya miongoni mwa baadhi ya nchi za Afrika zenye kuwa na idadi kubwa ya vijana wanaojitoa uhai. Makala haya yanaangazia safari ya nchi ya Kenya kuipa kipau mbele afya ya akili, na kuainisha baadhi ya juhudi za serikali ikiwemo kupitishwa kwa sheria ya afya ya akili pia ujenzi wa hospitali maalum ya kuwatibu wagonjwa wenye matatizo ya akili.