
Sign up to save your podcasts
Or


Mchungaji Cyprian Michael anatushauri juu ya uongozi wa familia na uongozi kanisani katika podcast hii. Badala ya kuongoza tukiwa peke yetu, anatuhimiza kulenga watu wenye sifa na uwezo wa kuongoza na kuwaandaa ili wawe bega kwa bega pamoja nasi katika uongozi na wawe tayari kushika uongozi wa huduma siku zijazo.
Mchungaji Emmanuel Mwankasole kutoka Dodoma, Tanzania anatukumbusha juu ya umuhimu wa kufanya uanafunzi. Baada ya kujibu swali la msingi "Kwa nini tufanye?" yeye anaendelea kutoa mafunzo mazuri sana kwa ajili ya viongozi, namna ya kufanya uanafunzi na faida tutakazoziona tukifanya uanafunzi kwa uaminifu. Bila shaka utabarikiwa na kujengwa na podcast hii.
Kiongozi D. Kitang'wa anatushauri kuhusu afya katika mwili wa Kristo. Ili afya ya kiroho iwe nzuri, inabidi sisi tulio viongozi wa kiroho tufundishe watu wetu vizuri. Haitoshi tu kuwafundisha kuepukana na dhambi ambazo zimekatazwa na Mungu katika Neno lake, lakini tunapaswa kuwafundisha kutii na kutenda tuliyoamriwa naye vilevile.
Sisi sote tuna mawazo yetu juu ya kanisa na uongozi katika kanisa, lakini mawazo yetu siyo sawa. Ni kwa sababu tumeathiriwa na mila na utamaduni pamoja na uzoefu wetu tangu utoto. Kuna aina mbalimbali za makanisa na namna tofauti tofauti za uongozi katika kanisa. Je, zote zinakubalika? Zote ni za kibiblia? Podcast hii na zingine zifuatazo zitahusu mada hii ya kanuni muhimu kutoka Neno la Mungu zinazotuongoza tuwe na kanisa la kibiblia na uongozi unaokubaliwa na Bwana.
Mzee Smith anazungumza na mchungaji ambaye, pamoja na kuongoza kanisa na kufanya huduma nyingine nyingi, anaweka mkazo katika kazi muhimu ya kulea viongozi wengine. Sikiliza mashauri yake namna ya kutambua viongozi wa siku zijazo na jinsi ambavyo mchungaji anaweza kuwafundisha na kuwalea katika kanisa.
Tuko na mkurugenzi wa Huruma Children’s Home katika podcast ya leo. Mzee Smith alikaa naye ili kumhoji juu ya ulezi wa watoto na vile ambavyo tunaweza kuwa wazazi bora katika ulezi wetu wa watoto. Usikose podcast hii ambayo imejaa hekima na mashauri mazuri kwa ajili yetu sisi tulio wazazi.
Katika podcast hii tunaendelea kujifunza kutoka kwa mfano wa Musa aliyepelekwa na Bwana jangwani kwa ajili ya mafunzo. Wakati ulipowadia atoke jangwani na kuingia katika huduma alikataa, akiona hawezi. Pengine wewe unatoa udhuru kama Musa. Tuone Mungu anasemaje juu ya kiongozi aliyeweza kutumiwa naye kutenda makuu.
Je, kiongozi mkuu ni yule ambaye ni mnenanji mzuri, ana talanta na vipaji vya pekee, na anasifiwa na watu? La, hasha. Katika mfano wa Mtumishi Musa tunaona kwamba mara nyingi ni kinyume. Kiongozi mkuu ambaye Mungu hupenda kumtumia ni yule ambaye amepita katika jangwa na kujifunza kuwa mwaminifu katika madogo, akimtegemea Bwana kwa unyenyekevu.
Tunamkaribisha Mzee Vernon Smith ambaye anajiunga na huduma ya podcast ya Uongozi wa Kiroho na atakuwa akichangia podcast mara kwa mara.
From the publisher's feed