Siha Njema

Utengano wa familia unaweza kuleta shinikizo la damu au kisukari


Listen Later

Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo  hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao.

Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita.

Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika .

Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe  na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili.

Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi.

Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au  kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka.

Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Siha NjemaBy RFI Kiswahili


More shows like Siha Njema

View all
Jaridun Duniya - RFI by RFI Hausa

Jaridun Duniya - RFI

0 Listeners

Archives d'Afrique by RFI

Archives d'Afrique

85 Listeners

Appels sur l'actualité by RFI

Appels sur l'actualité

22 Listeners

公民论坛 by RFI - 法国国际广播电台

公民论坛

5 Listeners

 by RFI Brasil

1 Listeners

 by RFI Kiswahili

0 Listeners

 by RFI Tiếng Việt

13 Listeners

 by RFI ខេមរភាសា / Khmer

2 Listeners

Marchés du monde by RFI

Marchés du monde

0 Listeners