Shirika la afya duniani, WHO, limesema maisha ya wanaume wengi yanafupisha kutokana na wao kuwa na maumbile dhaifu na kuishi maisha hatari ya kutokuwa makini na afya zao.
Mwezi Juni, ulimwengu hutenga juma moja kati ya tarehe 14 hadi 20 kuhamasisha jinsia ya kiume kuhusu afya zao, kwenye makala haya tunajadili kwa nini wanaume hawapendi kufanyiwa uchunguzi wa afya au kwenda hospitali.