Katika makala ya Siha Njema juma hili , ambapo dunia hutenga wiki ya kwanza ya Agosti kuwahamasisha akina mama kuwanyonyesha wanao kwa miezi sita ya kwanza katika maisha yao,tunaangazia juhudi za akina mama kunyonyesha wakati huu wa Covid 19 . Baadhi yao wameambukizwa Corona na kulazimika kujitenga na wanao wachanga.