Msimu wa kutolewa kwa tuzo umekaribia, tuzo za Grammy za mwaka 2019 imeshatangaza washindanishi katika vitengo tofauti. Wakati Cardi B na mme wake watangaza kuachana, Nicki Minaj atamuonyesha mpenzi wake mpya kwenye mitandao wa kijamii.
Mastaa mbalimbali toka pande zote duniani walikutana nchini Afrika Kusini katika maadhimisho ya tamasha la Global Citizen, ambalo lilimkumbuka rais Nelson Mandela ambaye mwaka huu angekuwa anafikisha miaka mia. Priyanka Chopra na Nick Jonas wafunga ndoa nchini India.
Mashindano ya urembo na tamasha za utambuzi na ueleo wa ulemavu wa ngozi yafana nchini Mali na Uganda. Na mwanamuziki wa Angola wa opera ang'ara katika matamasha ya duniani.
Leo katika Zulia Jekundu tuna makala maalumu ya kufikisha vipindi 200 . Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya walemavu ya Angola yatwaa kombe la dunia nchini Mexico.
Tuzo za muziki za MTV Ulaya zilizofanyika Ulaya zamalizika kwa wanawake kung'ara katika tuzo hizo. Mmoja wao ni Janet Jackson ambaye tuzo ya Global Icon, na Tiwa Savage kutoka Nigeria alijipatia tuzo ya Best of Africa .
Idris Elba atunukiwa wadhifa wa kuwa mwana mme mwenye mvuto kuliko wote duniani na Jarida la People. Filamu ya Bohemia Rhapsody ambayo ni historia ya maisha ya Freddie Mercury, ambaye jina lake halisi ni Farrokh Bulsara Mtanzania aliyezaliwa Stone Town Zanzibar na kuhamia England .