Babananiii

Babananiii

By Fabian C. MwakabanjeArtsBooks
Download on the App Store

Babananiii episodes

  • MKOPESHA PESA WA BABELI
    "Zawadi uliyopewa na mfalme inatakiwa kukufundisha hekima. Ukitaka kubaki na vipande vyako hamsini
    vya dhahabu, unatakiwa kuwa makini. Utavutiwa na vitu vingi na utapata ushauri mwingi sana.
    Utaambiwa fursa nyingi zinazodaiwa kutoa faida kubwa. Habari na hadithi kutoka kwenye sanduku langu
    la dhamana zinatakiwa kuwa onyo kwako. Kabla hujaruhusu pesa yako kutoka kwenye pochi hakikisha
    utaweza kuirudisha. Kama utahitaji ushauri zaidi unaweza kurudi nami nitafurahi kukupatia.
    '''Mwisho naomba usome nilichoandika. Chini ya mfuniko wa sanduku la dhamana. Maneno haya yana
    faida kwa mkopeshaji na mkopaji pia.
    Bora tahadhari kidogo kuliko majuto makubwa.
    32 min
  • ZIJUE SHERIA TANO ZA PESA
    "Ukiambiwa uchague kati ya mfuko uliojaa dhahabu na mabamba ya vigae yaliyoandikwa maneno ya
    hekima na busara, utachagua nini?"
    Wasikilizaji walikuwa wamekaa jangwani wakiwa wamekusanyika kuzunguka moto. Walikuwa
    wakisikiliza kwa makini. Mwanga wa moto ulionyesha nyuso zao ambazo zilianza kuwa nyeusi sababu ya
    jua la jangwani.
    "Dhahabu, dhahabu," walijibu wote ishirini na saba kwa pamoja.
    Mzee Kalabab alitabasamu kama vile kuna siri anaifahamu yeye peke yake.
    29 min
  • TIBA 7 ZA POCHI TUPU (4 - 7)
    Hizi ndizo jumla ya tiba saba za pochi tupu. Kwahiyo tiba ya saba na ya mwisho ya kutibu pochi tupu ni kuwa mtu bora. Kujifunza na kujizoeza kupata maarifa zaidi, kupata ujuzi zaidi na kujiendesha maisha yako kwa heshima. Hapo unaweza kujiamini na utaweza kutimiza malengo yako.
    27 min
  • TIBA YA PILI & TATU YA POCHI TUPU
    ''Utajiri wa mtu haupo kwenye fedha zilizopo kwenye pochi yake bali kwenye kijito cha dhahabu
    kinachotiririka kwenda kwenye pochi yake na kuitunisha. Kipato kinachoingia hata akisafiri au asipofanya
    kazi."
    12 min
  • TAJIRI WA BABELI (Sura ya Kwanza)
    MTU ALIYETAMANI DHAHABU. Sehemu ya Kwanza katika kitabu cha Tajiri wa Babeli inaongelea hadithi ya marafiki wawili; Bansir na Kobbi ambao walijiuliza kuhusu kupata mali na walifanya uamuzi wa kutafuta suluhu ya tatizo lao la ukata wa kila mara.
    18 min

About Babananiii

From the publisher's feed

A literate African empowering the community through literacy programs.