Dakika 10 Za Kocha

Dakika 10 Za Kocha

By Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.BusinessEntrepreneurshipEducationSelf-ImprovementInvesting
Download on the App Store

Dakika 10 Za Kocha episodes

  • #DZK094; Unakuwaje ‘Bize’ Na Matokeo Hayaonekani
    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK093; Hili Ndilo Eneo Pekee Ambalo Kamwe Siwezi Kukuamini.

  • #DZK092; Hiyo Siku Moja Ndiyo Sasa

  • #DZK091; Huhitaji Akili Kubwa Sana Kufanikiwa Kama Utaweza Kufanya Kitu Hiki Kimoja
    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK090; Tumia Sababu Hizi Kuendelea Hata Pale Unapokuwa Na Kila Sababu Za Kukata Tamaa
    #BZK090; Tumia Sababu Hizi Kuendelea Hata Pale Unapokuwa Na Kila Sababu Za Kukata Tamaa

    Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1009/

    Rafiki yangu Mpendwa,

    Mafanikio ni rahisi kuyasema na kuyapanga, lakini ni magumu mno kuyapata. Hiyo ndiyo sababu pamoja na wengi kutaka mafanikio, wachache sana ndiyo wanaoyapata.

    Na siyo kwamba wachache hao wanaoyapata mafanikio wana bahati sana au wana upekee ambao wengine hawana. Watu wote wanapitia mambo yale yale kwenye safari ya mafanikio.

    Hakuna safari ya mafanikio ambayo haikutani na magumu na changamoto. Watu wote wanaianza safari ya mafanikio kwa malengo na mipango mizuri. Lakini wanapoanza utekelezaji, ndiyo wanakutana na uhalisia, ambao hawakuwa wanaujua.

    Kila anayeianza safari ya mafanikio, anafika hatua ambayo anaona hawezi na wala hakuna sababu ya kuendelea tena na safari hiyo. Kila mtu anapokutana na magumu na changamoto, anajua kabisa kwamba lazima avuke hayo ndiyo afanikiwe. Na hilo linafundishwa sana, lazima mtu upambane, ung’ang’ane ndiyo ufanikiwe.

    Lakini kuna hii pointi ambayo huwa haizungumziwi sana. Pointi ambayo mtu anafikia na kuwa na ushahidi wa kutosha kwamba hana tena sababu ya kuendelea. Pointi ambayo mtu anaona amefanya kila kilichokuwa ndani ya uwezo wake na hakuna namna anaweza kuendelea tena.

    Hii ndiyo pointi ambayo wengi hukata tamaa na kuacha kufanya. Na hiyo ndiyo pointi inayowatofautisha wale wanaopata mafanikio makubwa na wanaobaki kawaida. Siyo kwamba wanaofanikiwa huwa hawafikii pointi hiyo ya kukata tamaa.

    Kila anayekuwa kwenye safari ya mafanikio anafikia hiyo pointi, lakini wanaofanikiwa wanaendelea japo kidogo tu. Na huko kuendelea kidogo tu ndiko kunakoleta mafanikio makubwa sana. Ni pointi moja ndogo ndiyo inayowatofuatisha wanaofanikiwa sana na wanaoshindwa.

    Kwenye hii #BaruaYaKocha unaenda kujifunza jinsi na wewe unavyoweza kuendelea japo kidogo tu pale unapofika kwenye hatua ya kukata tamaa. Utatoka hapa na mkakati wa kukuwezesha kuvuka nyakati ngumu sana za maisha yako na kuendelea kufanya, kitu kitakachokupa matokeo unayoyataka.

    Endelea kusoma barua hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1009/

    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK089; Mafanikio Yanataka Uzito, Lakini Dunia Inakuhadaa Na Wepesi
    #BZK089; Mafanikio Yanataka Uzito, Lakini Dunia Inakuhadaa Na Wepesi

    Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1008/

    Rafiki yangu Mpendwa,

    Tunaishi kwenye dunia inayokwenda kwa kasi kubwa sana. Maendeleo makubwa ya teknolojia yamerahisisha sana mambo yote ambayo binadamu tunayafanya.

    Mtu aliyefariki karne ya 19 na hata ya 20, akifufuka leo na kuona hatua ambazo zimepigwa, atadhani maisha ya watu yako vizuri sana. Lakini atakapopata nafasi ya kuangalia maisha halisi ya watu, ataona bado hayana tofauti kubwa na yale waliyoishi wao.

    Ujio wa Akili Unde (AI) umemwezesha kila mtu kuweza kufanya kitu chochote anachotaka. Hata kama mtu hana uwezo na ujuzi mkubwa, kwa kuweza kuielekeza vizuri AI, anaweza kupata matokeo asingeweza kuyapata yeye mwenyewe.

    Lakini pamoja na fursa hiyo kubwa ya kila mtu kuweza kufanya chochote anachotaka, bado swala la mafanikio limekuwa mtihani mgumu. Bado watu wanaofanikiwa wanabaki kuwa wachache, huku wengi wakiyatamani mafanikio, lakini wanashindwa kuyapata.

    Kila mtu sasa ana zana za kumwezesha kufanya chochote kitakachompa mafanikio anayoyataka. Lakini wengi wanashindwa kutumia zana hizo, kwa kutokujua kitu muhimu kuhusu mafanikio.

    Kitu hicho ni mafanikio kutaka sana uzito, wakati dunia inahadaa na wepesi. Hapo ndipo penye mtihani mkubwa. Wakati tuna zana nyingi za kurahisisha mambo, tunaishia kuyafanya kwa wepesi. Wakati huo, mafanikio bado yanataka uzito, ambao tunaweza kuupata kwa zana tulizonazo, ila siyo kwa urahisi kama tunavyotaka.

    Kwenye hii #BaruaYaKocha naenda kukukumbusha umuhimu wa uzito kwenye mafanikio na kukuongoza kutengeneza uzito ambao utakupa mafanikio makubwa. Na kwa zana nzuri zilizopo sasa, ukishauelewa uzito, inakuwa swala la muda tu kwako kupata mafanikio makubwa unayoyataka.

    Endelea kusoma barua hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1008/

    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK088; Hii Ndiyo Sababu Ya Maisha Yako Kutokubadilika Licha Ya Kupambana Sana Kujiboresha
    #BZK088; Hii Ndiyo Sababu Ya Maisha Yako Kutokubadilika Licha Ya Kupambana Sana Kujiboresha

    Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1006/

    Rafiki yangu Mpendwa,

    Eneo la maarifa na hamasa ya mafanikio kwa sasa lipo vizuri sana. Kila mtu anayetaka mafanikio kwenye jambo lolote lile, ana fursa nyingi za kujifunza na kuhamasika ili kufanikiwa.

    Siri zote za mafanikio kwa sasa zipo bayana. Hakuna tena kilichofichwa kuhusu mafanikio. Mtu yeyote anayetaka mafanikio, anaweza kujua chochote anachotaka kuhusu mafanikio hayo. Hakuna tena taarifa zinazohodhiwa na watu wachache.

    Hadithi za watu waliofanikiwa ni nyingi na za kuhamasisha na kusisimua. Kwa yeyote anatetaka mafanikio, zipo hadithi zinazoendana na yeye kabisa. Hadithi za watu walioanzia chini kuliko hata yeye, wakapitia magumu sana, lakini wakapambana na kufanikiwa.

    Pamoja na mambo hayo yote kuwa rahisi, bado wanaofanikiwa wanabaki kuwa wachache, huku wengi wakibaki kwenye hali za chini au wakijitahidi sana kuwa kawaida.

    Hii ni hali ambayo watu wengi wanaipitia, wanapambana sana kujiboresha, wanasoma kila kitabu wanachoambiwa, wanahudhuria semina na mafunzo mbalimbali. Wanachukua hatua kwenye yale wanayojifunza, lakini bado maisha yao hayabadiliki.

    Ni jambo ambalo linawaacha wengi wakiwa wamekwama, wasijue nini cha kufanya ili waweze kutoka kwenye mkwamo huu.

    Kwenye hii #BaruaYaKocha unaenda kujifunza sababu zinazokukwamisha kufanikiwa licha ya juhudi kubwa unazoweka kwenye kujiboresha. Kwa kujua sababu hizo na kuzifanyia kazi, juhudi zako zitaweza kuleta mabadiliko unayotaka.

    Endelea kusoma barua hii hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1006/

    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK087; Siri Nzuri Usiyoijua Kuhusu Nidhamu Binafsi
    *#BZK087; Siri Nzuri Usiyoijua Kuhusu Nidhamu Binafsi*

    Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1002/

    Rafiki yangu Mpendwa,

    Inapokuja kwenye mafanikio, nimekuwa nakusisitizia mambo mawili ya kujenga, tabia na nidhamu sahihi ya mafanikio. Huwa tunajenga tabia na kisha tabia zinatujenga, kwa sababu sehemu kubwa ya mambo tunayofanya kila siku tunaongozwa na tabia. Tukiweza kujenga tabia sahihi, sehemu kubwa ya safari ya mafanikio inakuwa imefanikiwa.

    Ili kujenga tabia sahihi, nidhamu inahitajika sana. Na hapo ndipo mtego mkubwa ulipo, kwa sababu kujenga nidhamu kunatutaka kujisukuma zaidi ya tunavyotaka sisi wenyewe. Nidhamu ni kutekeleza yale uliyopanga, kama ulivyopanga, iwe unajisikia au hujisikii. Nidhamu ni kubaki kwenye mpango wako na kuachana na hisia zako.

    Kwa sababu kwa asili sisi binadamu ni viumbe wa kihisia, tunaofanya mambo kwa kusukumwa na hisia, nidhamu imekuwa inaonekana ni kujitesa, kwa sababu inatutaka kwenda kinyume na hisia. Kwa kuona nidhamu ni mateso inakuwa kitu kigumu kujijengea.

    Kwenye barua hii tunaenda kuangalia upande wa pili wa nidhamu binafsi, ambao una siri nzuri ambazo wengi hawazijui. Wakati tunaangalia nidhamu kama kujitesa, tunashindwa kuona upande mwingine wa nidhamu ambao ni kujitengenezea mazingira bora zaidi.

    Endelea kusoma #BaruaYaKocha hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1002/

    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK086; Kwa Nini Umechagua Huu Utumwa Kwenye Ulimwengu Unaoweza Kuwa Huru?
    *#BZK086; Kwa Nini Umechagua Huu Utumwa Kwenye Ulimwengu Unaoweza Kuwa Huru?*

    Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1001/

    Rafiki yangu Mpendwa,

    Nimekuwa nakukumbusha sababu kuu mbili za maamuzi yote tunayofanya sisi binadamu. Sababu hizo zikiwa ni furaha na uhuru. Tunafanya maamuzi ili kuwa na furaha na kuwa huru zaidi. Hayo ndiyo mahitaji yetu ya msingi kabisa binadamu, ambayo tukiyatimiza, mengine yote yanakuwa sawa.

    Lakini sasa, cha kushangaza, maamuzi mengi tunayoyafanya yanatukwamisha kwenye kupata matokeo hayo mawili. Tunafanya maamuzi ambayo yanatunyima furaha na yanatukosesha uhuru. Kwa bahati mbaya sana, wakati tunafanya maamuzi hayo tunadhani yatatupa vitu hivyo. Ni mpaka matokeo yanapokuja kuonekana ndiyo tunagundua kwamba tumepoteza vitu hivyo badala ya kuvipata.

    Kibaya zaidi, kila tunapokazana kurekebisha makosa tuliyofanya, tunazidi kupotea zaidi. Tunapofanya maamuzi na kujikuta tumekosa furaha na uhuru, tunakimbilia kufanya maamuzi mengine ili kubadili hali hizo. Lakini matokeo yake ni tunazidi kukosa furaha na uhuru.

    Hayo yote yamekuwa yanatokea kwa sababu namna tunavyofanya maamuzi yetu mengi siyo sahihi. Tunafanya kwa kuiga na kwa mazoea, kitu kinachopelekea tupate matokeo yale yale ambayo ndiyo tusiyoyataka.

    Kwenye barua hii naenda kukuonyesha utumwa ambao umeuchagua mwenyewe, licha ya kuwa na uwezo wa kuishi kwa uhuru kamili kadiri ya unavyotaka. Kwa chochote unachoona ni kikwazo kwako, wewe mwenyewe ndiye uliyekisababisha.

    Endelea kusoma #BaruaYaKocha hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1001/

    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min
  • #DZK085; Kama Unaweka Malengo Na Huyatimizi, Tumia Huu Mbadala.
    *#BZK085; Kama Huwa Unaweka Malengo Na Huyatimizi, Achana Na Malengo Na Fanya Kitu Hiki*

    Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1000/

    Rafiki yangu Mpendwa,

    Imegundulika kwamba watu huwa wanaweka malengo yake yale, kila mwaka kwa mpaka miaka 10 bila kutekeleza. Yaani imekuwa ni kama fasheni, kila mwanzo wa mwaka watu wanaweka malengo na kuamini mwaka huo wanaenda kufanya makubwa.

    Lakini muda unavyokwenda, malengo mengi yanasahaulika na kutokutekelezwa. Baadaye mtu anaona muda umeenda na kusubiri mwaka mwingine mpya ili aweke upya malengo yake. Hivyo ndivyo watu wamekuwa wanayaendesha maisha yao na kushangaa kwa nini hawafanikiwi.

    Hivyo ndivyo tunapata watu wanaosema kila mwaka wataanza biashara au kukuza na hawafanyi hivyo. Kila mwaka wanasema wataanza kuweka akiba na kuwekeza kwa msimamo bila kuacha, lakini hawafanyi.

    Najua wewe ni mmoja wa watu ambao hurudhiki na namna unavyoenda na malengo unayojiwekea. Najua umeshakazana sana kuweka malengo, lakini mengi umekuwa huyatimizi kama ambavyo umekuwa unayaweka.

    Hilo siyo tatizo lako tu, ni tatizo la kila mmoja wetu. Na tatizo hilo linachangiwa na namna tunavyoyachukulia malengo. Kwenye barua hii tunaenda kuangalia tatizo la malengo na mbadala wake ili tuweze kupata mafanikio makubwa tunayoyataka.

    Endelea kusoma #BaruaYaKocha hapa; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter-content/4/1000/

    Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.

    Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

    Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

    Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.

    Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
    1. MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
    2. FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
    3. BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
    Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
    1. #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
    2. #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
    3. #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
    Karibu ujifunze.
    11 min

About Dakika 10 Za Kocha

From the publisher's feed

Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka…