Acha Kufanya, Anza Kujenga.
Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills....
Rafiki,
Unaweka juhudi kubwa sana kila siku,
Unafanya kwa muda mrefu,
Unapata matokeo ya muda mfupi,
Lakini hupati mafanikio makubwa unayoyataka.
Siyo bahati mbaya,
Na siyo kwamba mafanikio hayawezekani kwako.
Bali unachohangaika nacho ndiyo hakiwezi kukupa mafanikio unayotaka.
Unahangaika na kufanya, badala ya kujenga.
*Unafanya biashara, badala ya kujenga biashara.*
Ndiyo maana biashara inakupa faida ukiwepo,
Ila usipokuwepo haiwezi kwenda.
Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha *jinsi ya kutoka kwenye ufanyaji na kwenda kwenye ujengaji.*
Soma barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills....
Imetosha sasa kufanya, anza kujenga upate mafanikio makubwa.
Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya
MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO. Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika.
Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu;
- MAFANIKIO; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio.
- FEDHA; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha.
- BIASHARA; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea.
Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi;
- #BaruaZaKocha; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/
- #OngeaNaKocha; https://www.youtube.com/@onkocha
- #AmkaNaKocha; https://amkamtanzania.com/
Karibu ujifunze.