Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Sehemu ya kwanza mjadala kuhusu malengo endelevu ya umoja wa Mataifa
    Mtangazaji wa makala haya juma hili anaangazia malengo endelevu ya umoja wa Mataifa ambayo yako takribani 17 wakati huu mkutano mkuu wa umoja wa Mataifa ukiwa unafanyika. Je malengo haya ya mwaka 2030 yatafikiwa na nchi nyingi duniani? Mjadala wetu leo unajikita hapa, mtangazaji amewaalika Dr Wetengere Kitojo mtaalamu wa uchumi na mhadhiri katika chuo cha Diplomasia na Julius Kiting'ati yeye ni balozi wa malengo endelevu ya umoja wa Mataifa.
    10 min
  • Athari za kiuchumi za ongezeko la watu duniani
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 11 ya mwezi Julai, kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni kuhusu kuhamasisha uzazi wa mpango, kuwawezesha watu na kuleta maendeleo ya nchi.
    Mtayarishaji wa makala hii, amezungumza na mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dr Wetengere Kitojo kuangazia athari za kiuchumi za ongezeko la idadi ya watu kwenye nchi na namna bora ya kudhibiti ongezeko la watu kwa kwenda sambamba na ukuaji na mgawanyo wa rasilimali za nchi.
    10 min
  • Tatizo la ajira kwa vijana na namna viongozi wa Au wanavyojaribu kukabiliana nalo
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia kilichojiri kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika waliokuwa wanakutana jijini Addis Ababa Ethiopia, ambapo moja ya suala lililojadiliwa kwa kina ni tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na kusaka mikakati ya kukabiliana na janga hili.
    Mtayarishaji wa makala hii amezungumza na Naamala Samson, mwanaharakati wa masuala ya vijana na Meneja mafunzo kutoka shirika la kimataifa la maendeleo ya vijana BRAC nchini Tanzania.
    10 min
  • Ubunifu wa mafazi unavyoweza kuongeza pato la mtu na kukuza uchumi
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, imekutana uso kwa uso na mbunifu maarufu wa nguo nchini Tanzania, Manju David Msita, mbunifu mkongwe anaefanya kazi ya kipekee katika ubunifu wa mavazi, anasema yeye haigi lakini ana buni.
    Mtayarishaji wa makala haya Emmanuel Makundi amezungumza na Manju kwa kina kuhusiana na sanaa ya ubunifu na namna inavyoweza kutumiwa na wabunifu hasa vijana kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi kupitia sanaa hii.
    Waweza kuwasiliana na Manju Msita kwa Instgram/Facebook na barua pepe, [email protected]/ [email protected] au kwa namba +255 0655 411 441
    11 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners