Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Kuzuia mchanga wa madini kusafirishwa kwenda nje ya nchi, je kutainufaisha Tanzania
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia kwa kina hatua ya Serikali ya Tanzania, kupiga marufuku kusafirishwa nje ya nchi kwa mchanga wowote wa madini kwaajili ya kwenda kuchanjuliwa. Badala yake Serikali inasema inaandaa utaratibu kuhakikisha inaupima kujua ni kiasi gani cha madini kilichomo.
    Wataalamu wa masuala ya uchumi na wachimbaji wenyewe wanamtazamo gani? Ungana na mtayarishaji wa makala haya kufahamu mengi.
    11 min
  • Ujenzi wa reli za kisasa kwenye nchi za Afrika Mashariki
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia namna ambavyo nchi wanachama za Afrika Mashariki zimeanza harakati za kukamilisha ujenzi wa reli za kisasa kuunganisha mataifa yao, Kenya wanaelekea kumaliza na Tanzania na Uganda zinaelekea kuanza, lakini nini faida ya reli hizi za kisasa? Mtangazaji wa makala haya amezungumza na Dr Wetengere Kitojo, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Dar es Salaam, Tanzania pamoja na wananchi wa Kenya.
    10 min
  • Namna sanaa ya uchoraji inavyoweza tumika kukuza uchumi
    Juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi, mtangazaji wa makala haya amezungumza na msanii anayechora vibonzo Mohamed Jumanne maarufu kwa jina la kisanii kama Dr. Meddy, wamezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna sanaa hii inavyoweza kutumika kukuza kipato cha mtu na kuchangia kwenye pato la taifa.
    11 min
  • Ziara ya rais wa Uganda nchini Tanzania na kwanini hawajasaini mkataba wa EPA
    Mtangazaji wa makala haya juma hili amezungumzia ziara ya rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni nchini Tanzania, ambako alikutana na mwenyeji wake John Pombe Magufuli.
    Wamezungumza mengi viongozi hawa lakini kubwa ni biashara baina ya nchi hiyo mbili pamoja na mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na nchi za Ulaya maarufu kama EPA, mkataba ambao Tanzania na Uganda bado hazijautia saini.
    10 min
  • Uganda yazindua kiwanda cha kusafisha dhahabu, Serikali yatangaza kuondoa mirabaha
    Mtangazaji wa makala haya juma hili amzungumza na mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dr Wetengere Kitojo, ambapo amezungumzia umuhimu wa nchi wananchama za Afrika Mashariki kuanzisha viwanda vya ndani vya kuchakata bidhaa na kuzipa thamani kabla ya kuuzwa nje ya nchi, Jumatatuj ya tareh 20 nchi ya Uganda ilizindua rasmi kiwanda cha kusafisha dhahabu, lengo likiwa ni kujaribu kupunguza wimbi la biashara haramu ya dhahabu kwenye masoko ambayo sio rasmi.
    11 min
  • Athari ya biashara ya dawa za kulevya kwa uchumi na maendeleo ya nchi
    Mtangazaji wa makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili amezungumza na mtaalamu wa masuala ya uchumi Dr Wetengere Kitojo, ambapo wameangazia athari za kiuchumi kwa nchi hasa kutokana na kuendelea kwa biashara haramu ya dawa za kulevya kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
    Ndani ya makala haya utasikia uchambuzi wa kina kuhusu namna ambavyo biashara hii inaathiri uchumi, mzunguko wa fedha, jamii na ukuaji wa maendeleo.
    11 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners