Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Sehemu ya 2, mjadala kuhusu utandawazi na ukuaji wa uchumi
    Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inakuletea sehemu ya pili ya mjadala ulianza juma lililopita, kuhusu Utandawazi, je utandawazi umesaidia kukuza uchumi wa dunia na kuleta maendeleo au umezidisha ombwe la walio nacho na wasio nacho?
    Mtayarishaji wa makala haya, amezungumza na Profesa Hamfrey Moshi, mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Dar es Salaam, Tanzania, pamoja na Dr. Wetengere Kitojo mtaalamu wa uchumi na muhadhiri katika chuo cha diplomasia cha nchini Tanzania.
    11 min
  • Seheumu 1: Utandawazi umeleta mabadiliko ya kiuchumi au unaendelea kubomoa
    Mtangazaji wa makala haya, juma hili amezungumza na wataalamu wa masuala ya uchumi, katika sehemu ya kwanza ya mjadala kuhusu "Utandawazi", na swali la msingi ni je, Utandawazi umesaidia kuimarisha uchumi wa dunia, ama ni wachache tu wanaonufaika na maendeleo ya utandawazi? Ungana na mtayarishaji wa makala haya akizungumza na Profesa Hamfrey Moshi na Dr Wetengere Kitojo.
    9 min
  • Rais Obama amefanikiwa kiasi gani kuisaidia nchi yake na bara la Afrika kiuchumi
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia hotuba ya mwisho ya rais wa Marekani Barack Obama, aliyoitoa usiku wa kuamkia Jumatano ya Januari 11 barani Afrika, ambapo kubwa ni sera yake ya ushirikiano wa kimataifa na hasa kiuchumi na nchi za Afrika na mustakabali wa baadae wa Marekani baada ya rais mteule Donald Trump kuchukua madaraka rasmi.
    Mtangazaji wa makala haya, amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi, Dr Wetengere Kitojo, kutathmini ni kwa kiasi gani rais Obama amefanikiwa na sera yake ya kimataifa kuhusu uchumi na biashara.
    10 min
  • Watumiaji wa simu Tanzania kuanza kutozwa kodi ya ongezeko la thamani
    Mtangazaji wa makala haya, juma hili ameangazia hatua ya kampuni za mawasiliano ya simu nchini Tanzania, kuanza kutoza wateja wao, kodi ya ongezeko la thamani, VAT, katika vocha watakazokuwa wananunua na kutumia kwa mawasiliano yao.
    Hatua hii itaathiri vipi watumiaji wa simu? Ni kweli Serikali kunufaika na hatua hii kupitia marekebisho ya kodi waliyoyafanya? Kwa makampuni yenyewe hali itakuwaje? Ungana na mtangazaji wa makali haya akidadavua suala hili kwa kina na wataalamu wa uchumi.
    10 min
  • Ripoti ya UNDP kuhusu usawa wa kijinsia na maendeleo barani Afrika
    Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia namna ambavyo kukosekana kwa usawa wa kijinsia, kunavyoligharimu bara la Afrika kiasi cha dola za Marekani bilioni 105 kila mwaka.
    Je, nini kifanyike ili kufikia malengo ya milenia na yale ya malengo endelevu kuhusu usawa wa kijinsia? ungana na mtangazaji wa makala haya kupata uchambuzi wa kina.
    11 min
  • Kizungumkuti kuhusu ufadhili wa fedha kwa bara la Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
    Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili imeangazia yanayojiri kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, CP22, unaofanyika mjini Marrakech, Morocco, ambako mataifa yanakutaja kujadili na kuanza kutekeleza mkataba wa Paris uliotiwa saini mwaka uliopita.
    Nchi zilizoendelea ziliahidi kulichangia bara la Afrika kiasi cha fedha ili kuziwezesha kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini bado mvutano ni mkubwa kuhusu masharti na namna fedha hizo zinavyotolewa, huku wataalamu wakionya uchumi wa dunia kuteteraka ikiwa nchi hazitakubaliana sasa.
    10 min
  • Ushindi wa Trump unaashiria nini kwa uchumi wa dunia
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia ushindi wa mgombea wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, ambaye amemuangusha vibaya mgombea wa Democrat, Hillary Clinton, ambaye amekubali kushindwa.
    Ushindi wa Donald Trump unaashiria nini kwa uchumi na usalama wa dunia? ungana na mtayarishaji wa makala haya kufahamu mengi.
    10 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners