Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Nini nafasi ya Afrika Kusini kwenye uchumi wa nchi za EAC
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia ziara ya Rais wa Afrika Kusini nchini Kenya, Jacob Zuma. Ni ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na kiongozi wa Afrika Kusini aliyeko madarakani nchini Kenya. Mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ilitiwa saini na wakuu wa nchi hizi mbili.
    Ziara hii ina umuhimu gani kwa nchi ya Kenya na Afrika Kusini? Ungana na mtayarishaji wa makala haya akizungumza na mtaalamu wa masuala ya uchumi kuitathmini ziara hii.
    10 min
  • Nchi ya DRC na Tanzania zakubaliana kushirikiana kiuchumi
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia ziara ya Rais wa DRC, Josephu Kabila nchini Tanzania, ambapo alikutana na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli.
    Kwenye mazungumzo yao, viongozi hawa walikubaliana kushirikiana kiuchumi ambapo walitiliana saini mikataba ya ushirikiano. Uhusiano wa nchi hizi mbili utakuwa na manufaa gani kiuchumi?
    10 min
  • Sehemu ya pili kuhusu hatua ya wakuu wa nchi za EAC kutotia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na EU, maarufu kama EPA
    Kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunaendelea na mazungumzo yetu sehemu ya pili, kuhusu uamuzi wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutotia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya yao na ile ya umoja wa Ulaya, wataalamu wa masuala ya uchumi na hata baadhi ya wabunge wa bunge la Ulaya wanasema mkataba huu yafaa urekebishwe kwanza kabla ya kutiwa saini sababu hautakuwa na manufaa yoyote kwa viwanda vya ukanda.
    Tunaendelea na mahoano kati ya profesa Hamfrey Moshi, mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka Dar es Salaam, Tanzania.
    10 min
  • Wachumi; mkataba wa kiuchumi kati ya Ulaya na EAC haufai
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunakuletea uchambuzi wa sehemu ya kwanza ya kilichojiri baada ya mkutano wa dharula wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliokutana jijini Dar es Salaam, September 8, ambapo pamoja na mambo mengine walikataa kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Jumuiya yao na ile ya umoja wa Ulaya, wakijipa muda zaidi wa kupitia mkataba huo kwa miezi mitatu kabla ya kuamua ikiwa watie saini au la.
    11 min
  • Dodoma kuwa mkoa wa kiuchumi baada ya Serikali kuhamia
    Juma hili makala ya Gurudumu la Uchumi inakuletea makala maalumu kuhusu mkoa wa Dodoma na fursa za kiuchumi zinazopatikana kwenye mkoa huo ulio katikati mwa nchi ya Tanzania, ambapo Serikali ya awamu ya tano imepanga kuwa imehamishia wizara zake zote kwenye mkoa huol ambao unakuwa makao makuu rasmi ya nchi.
    8 min
  • Nchi za Afrika kunufaika na mkutano wa TICAD uliomalizika nchini Kenya
    Msikilizaji juma hili makala ya Gurudumu la Uchumi, inaangazia kutamatika kwa mkutano wa kimataifa wa kibiashara kati ya bara la Afrika na nchi ya Japan, ambapo mikataba ya maelewano zaidi ya 73 ilitiwa saini na Serikali ya Japan kukubali kulisaidia bara hilo kwa kutoa zaidi ya dola za Marekani bilioni 10 katika kipindi cha miaka 3.
    Nchi za Afrika zinanufaika nini kutokana na ushirikiano huu? Ungana na mtayarishaji wa makala haya Emmanuel Makundi akizungumza na Dr Wetengere Kitojom mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Dar es Salaam, Tanzania.
    10 min
  • Vita Sudan Kusini vyaendelea kudumaza uchumi wa taifa hilo jipya kabisa duniani
    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, imeangazia hali tete ya uchumi wa Sudan Kusini, ambao umeendelea kutatizika kutokana na mapigano ambayo yanaendelea kushuhudiwa nchini kati ya wapiganaji wa Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar.
    Mapigano haya yanaliweka taifa hili katika hali gani? Mtangazaji wa makala haya amezungumza na mchambuzi wa masuala ya uchumi na mtaalamu wa masuala ya diplomasia.
    10 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners