
Sign up to save your podcasts
Or


Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya.
Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?
Katika maeneo mengi nchini, hasa magharibi mwa Kenya, wasichana wengi wanaojikuta wakisuasua katika mitihani ya sekondari huishia kwenye ndoa za mapema na mimba za utotoni—mazingira yanayozima ndoto zao kabla hata hazijachanua. Lakini safari hii, upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma. Serikali za majimbo, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), zimeanzisha mpango wa mafunzo ya kitaaluma yanaotumia teknolojia ya kisasa, Lengo likiwa ni moja tu, kuwainua wasichana hawa.
Msikilizaji katika uhalisia mgumu wa maisha ya wakazi wa Goma, hususan baada ya mji huo kuangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, imeibuka hadithi ya kipekee ya uvumilivu na ubunifu wa wanawake.
Kati ya changamoto za ukosefu wa ajira na kuyumba kwa uchumi wa familia, wanawake kwenye mji huo wamegeukia ujuzi wa jadi wa kutengenezaji wa kinywaji cha asili kinachoitwa Mandale.
Mkataba wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani maarufu kama AGOA umefika tamati, ni mkataba uliokuwa unatoa fursa kwa nchi za Afrika kufikia soko la Marekani bila vikwazo vya kiushuru, bara hili likitengeneza faida ya mabilioni ya dola kupitia mkataba huu, hata hivyo kukoma kwake tayari kunashuhudiwa athari yalke kwenye baadhi ya nchi, kuanzia katika viwanda vya nguo nchini Kenya hadi kwa wasafirishaji huko Ghana, maisha ya watu walioajiriwa kupitia mkataba huu yako mashakani.
Msikilizaji katika nchi zote za Afrika Mashariki, kuna wimbi jipya la matamanio kuhusu hali ya biashara, vijana, wakiongozwa na ubunifu na ustahimilivu! Wakigeuza harakati zao kuwa biashara zinazostawi, kubadili changamoto kuwa fursa na ndoto kuwa ukweli.
Tutazungumza na Andrew Lukuwi, yeye ni mjasiriamali kijana akiwa nchini Tanzania, pamoja na Dr Onesmo Kyauke mchambuzi wa masuala ya uchumi na siasa akiwa Tanzania.
Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu mkubwa wa rasilimali fedha? Tutakuwa na wataalamu Walter Nguma na Dr Ponsian Ntui.
Leo hii tunatupia jicho uchumi wa bluu, eneo la kiuchumi linalotajwa kama suluhisho jipya la maendeleo endelevu, kukuza ajira na ubunifu, hata hivyo chini ya uso wa maji, maswali magumu yanajitokeza: Je, tunawekeza kimkakati kwa kuzingatia pia jamii zinazozunguka maeneo haya?
Tutazungumza na Dr Ponsian Ntui mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini mwanza nchini Tanzania, maarufu kama SAUT.
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunazungumzia mabadiliko makubwa ya kiuchumi kuhusu namna malipo ya kidijitali yanavyochochea huduma jumuishi za kifedha, ukuaji wa uchumi, na mageuzi ya kidijitali kwenye nchi za Afrika.
Wageni wetu leo ni Ali Mkimo mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, pamoja na Lucy Nshuti Mbabazi, mkurugenzi wa taasisi ya Better Than Cash Alliance iliyochini ya shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP.
Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, na kwingineko, ukosefu wa ajira kwa vijana umesalia kuwa wa kiwango cha juu, wakati huu maelfu ya vijana wakihitimu vyuo vikuu kila mwaka.
Bado tuko na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania, pamoja na Kamala Dickson kutoka asasi ya Agenda Participation Initiative ya nchini Tanzania.
Msikilizaji leo tunalijadili swali ambalo linaathiri mamilioni ya vijana katika ukanda wa Afrika Mashariki, pamoja na wageni tutajiuliza, Je, mfumo wa elimu unawaandaa vijana kupata ajira ambazo hazipo tena? Au tunakosa fursa katika sekta zinazoibukia kama vile teknolojia na uchumi bunifu?
Tutakuwa na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania, pamoja na Kamala Dickson kutoka asasi ya Agenda Participation Initiative ya nchini Tanzania.
From the publisher's feed
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

2 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners