Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Sehemu ya II: Mfumo mbovu au mafanikio, matajiri 4 Afrika kumiliki nusu ya mali za raia wa bara hilo

    Bar ala Afrika ni tajiri kwa rasilimali, vipaji na uwezo, hata hivyo, mamilioni ya raia wake bado wamenasa katika lindi la umaskini, huku wachache wakilimbikiza mali zisizomithilika, Je, hii inasema nini kuhusu sera, vipaumbele na mustakabali wa bara la Afrika?

    Hivi leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tutajadili tumefikaje hapa, ina maana gani kwa maendeleo na nini kinapaswa kubadilika kujenga uchumi wa haki na shirikishi?

    10 min
  • Sehemu ya I: Mfumo mbovu au mafanikio, matajiri 4 Afrika kumiliki nusu ya mali za raia wa bara hilo

    Katika bara lenye watu zaidi ya bilioni 1.4, ni watu wanne tu wanaomiliki utajiri zaidi ya nusu ya watu wote. Kulingana na ripoti mpya ya Oxfam, ukosefu huu wa usawa unaostua sio tu takwimu - ni ishara ya wazi ya ukosefu wa haki za kiuchumi uliokita mizizi, mifumo iliyovunjika na kukosekana kwa fursa.

    Kujadili haya yote nimewaalika Johnson Denge mtaalamu wa uchumi akiwa Nairobi na Apronius Mbilinyi yeye ni mtaalamu wa masuala ya Kodi akiwa Tanzania.

    11 min
  • Nchi zinazoendelea kulemewa na madeni: Je, Dunia itasikia kilio chao?

    Hivi Leo tunaangazia suala nyeti linalogusa maisha ya mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea hususani za bara la Afrika, kama vile kwenye mzigo wa madeni unaozidi kuwa mzito.

    Tunajiuliza Nini hasa kiko hatarini? suluhisho gani linapendekezwa? Kujadili hili tunazungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

    10 min
  • Utakatishaji Fedha: Kenya yawekwa kwenye orodha ya nchi zilizo na changamoto, Uganda ikiondolewa.

    Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo.

    Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha.

    Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine.

    Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.

    10 min
  • EAC: Vipau mbele vya Bajeti za Afrika Mashariki na maana yake kwa raia

    Alhamisi ya Juni 12, nchi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki kwa pamoja kupitia Mawaziri wa Fedha, waliwasilisha Bajeti ya mwaka wa fedha ya mwaka 2025/26.

    Waziri wa fedha John Mbadi aliwasilisha Bajeti ya Shilingi za nchi hiyo Trilioni  4.2. Bajeti ya Tanzania kwa mwaka huu wa fedha ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 56.49 huku Bajeti ya Uganda ikiwa ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 72.3.

    Lakini bajeti hii ina maana gani kwa raia wa nchi hizo na je bajeti hizi zinatoa taswira halisi ya mikakati yao nchi hizo kujitegemea na pia kukua? Skiliza makala haya upate ufahamu zaidi tukizungumza pia na David Otieno, mtafiti wa masuala ya bajeti kutoka shirika la Amnesty International.

    10 min
  • Mfumuko wa bei na mzigo wa madeni

    Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii tunajadili namna mfumuko wa bei na mzigo wa madeni umeendelea kuziathiri nchi zinazoendelea na namna gani zinaweza kukabiliana na changamoto hii.

    11 min
  • Sehemu ya II: Sehemu ya I: Je, Teknolojia Inaweza Kupunguza changamoto za Biashara barani Afrika?

    Msikilizaji wiki iliyopita katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tulianza na sehemu ya kwanza ya mada kuhusu namna teknolojia inavyoweza kuhusihwa kwenye biashara kutatua changamoto zinazolikabili bara la Afrika, ikiwemo biashara ya kidijitali kuchochea utangamano, kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo.

    Leo nakuletea sehemu ya pili ya mazungumzo yangu na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

    10 min
  • Sehemu ya I: Je, Teknolojia Inaweza Kupunguza changamoto za Biashara barani Afrika?

    Leo Katika makala ya gurudumu la uchumi tunakuletea sehemu ya kwanza ya mada kuhusu namna teknolojia inavyoweza kuhusihwa kwenye biashara kutatua changamoto zinazolikabili bara la Afrika, ikiwemo biashara ya kidijitali kuchochea utangamano, kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo.

    Leo nakuletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo yangu na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

    10 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners