
Sign up to save your podcasts
Or


Katika makala ya Gurudumu la Uchumi juma tunajadili athari za kibiashara kimataifa kutokana na hatua ya hivi karibuni ya Marekani kutangaza vikwazo vya kikodi kwa mataifa ya Canada, Mexico, India na Uchina ambao ni washirika wake wakubwa kibiashara.
Kujadili hili, kwenye line ya simu tunaungana na Profesa Wetengere Kitojo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Msikilizaji juma lililopita tulianza kwa kujadili yaliyotokana na mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, na suala kuu lilikuwa ni je, nchi za Afrika zitafanikiwa kushinikiza mabadiliko katika taasisi za kifedha za kimataifa na kuondokana na mikopo na madeni yasiyostahimilika ?
Leo katika makala ya Gurudumu la Uchumi, nakuletea sehemu ya pili ya mjadala huu, nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu namchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa nchini Tanzania.
Msikilizaji mwishoni mwa wiki iliyopita, viongozi wa Afrika waliokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, walikubaliana kuongeza kasi ya kudai mabadiliko kwa mifmo ya kifedha ya kimataifa, ili kuziwesha kuwa na nafasi katika maamuzi. Afrika inalalamika kutokuwepo usawa, na hivyo kuyaweka mataifa ya Afrika katika hali ya kutegemea mikopo yenye masharti magumu.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili ikiwa azma hii ya viongozi wa Afrika itafanikiwa.
Hujambo msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu, makala ni Gurudumu la Uchumi na leo hii tunazungumzia kuhusu athari za kiuchumi kutokana na mizozo kwenye nchi za Afrika.
Tutazungumza na Hamduni Marcel, mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.
Juma hili katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili kuhusu athari za hatua ya Marekani kusitisha kwa muda utoaji wa misaada ya nje. Uamuzi huu tayari umeonekana kutishia baadhi ya sekta zilizokuwa zinasaidiwa kupitia USAID kama vile Afya na Elimu.
Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Juma hili viongozi wa nchi za Afrika walikutana Tanzania, kujadili namna bora ya kuhakikisha raia wake wanaunganishwa na nishati ya uhakika, endelevu na nafuu ifikapo mwaka 2030.
Takwimu zinaonesha raia zaidi ya milioni 600 hawana umeme, bilioni 1 hawatumii nishati safi na salama.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, kuangazia changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa nishati, fursa zilizopo.
Msikilizaji ripoti mpya ya shirika la kupambana na umasikini Oxfam, inaonesha kuwa utajiri wa mabilionea uliongezeka mara tatu zaidi katika mwaka uliopita, ikiwa ni zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2023.
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tumezungumza Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara, kuangazia kwa kina ripoti hii na athari ya kuendelea kushuhudiwa kwa pengo la matajiri na masikini.
Teknolojia bunifu ya biashara ndogo ndogo imekuwa ikijulikana kuwa ya watu waliojiweza katika jamiii kutokana na gharama yake ,hali ambayo inawafungia nje watu hasa vijana kutoka maeneo duni na vijijini hivyo kukosa kuimarika kibiashara na kiuchumi kupitia teknolojia hizo .Lakini hata hivyo vijana pamoja na mashirika mbalimbali mtaa wakibera jijini Nairobi Kenya wapata fursa ya mafunzo na kuimarika kibiashara
Hivi leo ni sehemu ya pili ya makala ya Gurudumu la Uchumi, hasa tunapouanza mwaka 2025 tunaenda kujadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha, ufanye nini kuongeza kipato, unatumiaje fedha ulizonazo kuwekeza ? Haya ni baadhi ya mambo ambayo tutaenda kuyatazama kwenye makala ya juma hili. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Heri ya mwaka mpya 2025 msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu na hasa makala ya Gurudumu la Uchumi, ni imani yetu kuwa nyote mbuheri wa afya. Makala ya Gurudumu la Uchumi, tutajadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha. Kuzungumzia hili msikilizaji kwenye line ya simu nimemualika Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
From the publisher's feed
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

2 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners