
Sign up to save your podcasts
Or


Katika makala ya hivi leo, tunajadili kuhusu umuhimu wa kuwa na nidhamu ya fedha, kwanini ipo haja ya kuwa na nidhamu ya matumizi binafsi, vipi unaweza kujipanga kwa mwaka ujao? Haya ni miongoni mwa maswali ambayo mtaalamu wetu wa uchumi na biashara Ali Mkimo anaenda kuyajibu.
Makala haya yanazungumzia hatua za wanawake na wasichana katika eneo la Opapo, Kaunti ya Migori nchini Kenya, kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ya kaunti, wameanzisha kiwanda cha kuchakata samaki, kuboresha biashara ya samaki, na kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa kama soseji na baga,hivyo kuinua uchumi
Msikiliza mataifa 54 ya Afrika yametia saini mkataba wa biashara huria barani Afrika, mataifa 48 yakitia saini itifaki kuanza kuutekeleza. Huu ni moja ya mikataba mikubwa ya kibiashara duniani, ukitarajiwa kuwaondoa raia milioni 30 kutoka kwenye umasikini na kuongeza mapato ya bara hil hadi kufikia dola bilioni 450 ifikapo mwaka 2030.
Kuangazia kwa kina mkataba huu pamoja na hali ya madeni ya nchi za Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.
Msikilizaji kwa muda sasa, eneo la pwani ya Kenya limekuwa likikabiliwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, Hali hii ikichangia vitendo vya utovu wa nidhamu, kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na ndoa za mapema. Hata hivyo, kutokana na juhudi za mashirika mbalimbali ya kijamii na yasiyo ya kiserikali, vijana wengi walioacha kutumia dawa za kulevya sasa wanajihusisha na miradi ya kibiashara ili kujikimu.
Makala ua Gurudumu la Uchumi juma hili, inawaangazia vijana wa eneo la Pwani ambao wameamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Msikilizaji kwa muda sasa mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, kuanzia katika kukusanya mapato na matumizi kwa ajili ya maendeleo yake, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika urejeshaji.
Lakini je, kuongza kodi ndio suluhu? Mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Tanzania, Ali Mkimo anafafanua.
Mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, katika kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika ureje shaji.
Lakini je, kuongeza wigo wa kodi kwa mataifa yanayoendelea ndio njia pekee kuwezesha mataifa haya kujikwamua kiuchumi? Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tananzania
Msikilizaji dunia inashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miongo 6 iliyopita, ambapo mwaka 1960 idadi ilikuwa bilioni 3 lakini katika miongo miwili tu hadi mwaka 1982 ilikuwa imevuka watu bilioni 5 na November mwaka 2022 kulikuwa na watu bilioni 8 duniani.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunajadili Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa.
Tumezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania
Tatizo la fedha haramu barani Afrika linaligharibu bara hili kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 na bilioni 80 kila mwaka, Asilimia 44 ya utajiri wa kifedha wa Afrika inadhaniwa kuwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Uwazi wa Ushuru barani Afrika ya 2023, nchi za Afrika zimeokoa dola bilioni 2 kwa mwaka kutokana na watu kuweka wazi mapato yao, ubora wa kubadilishana taarifa na uchunguzi wa nje ya nchi.
Tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Msikilizaji kwa mujibu wa benki ya dunia, ni asilimia 49 tu ya watu wazima wanamiliki akaunti benki, takwimu za hivi karibuni zikionesha ongezeko la asilimia 55 mwaka 2021 kutoka asilimia 43 mwaka 2017, hata hivyo kiwango hiki kikiwa kidogo ukilinganisha na wastani wa kidunia wa asilimia 76.
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili tunajadili kuhusu huduma jumuishi za mifumo ya kifedha barani Afrika. Machambuzi wa masuala ya uchumi ALI MKIMO anajibu maswali kadhaa kuhusu sekta hii.
Msikilizaji juma lililopita Rwanda ilikuwa mwenyeji wa kongamano la mfumo wa chakula barani Afrika, ambapo wadau zaidi ya elfu 4 kutoka kila pembe ya mataifa ya Afrika walishiriki.
Mkutano uliangazia kuhusu mifumo ya chakula, mbinu bora na teknolojia ambazo zinaweza kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula barani Afrika na wakati huohuo kutengeneza nafasi za kazi na fursa kwa wanawake.
Msikilizaji wiki hii nimeshirikiana na mwanahabari wetu wa Kigali, Christopher Karenzi;
From the publisher's feed
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

2 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners