
Sign up to save your podcasts
Or


Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, wito umeendelea kutolewa na mataifa ya Afrika kuhusu kuwepo usawa na haki katika mfumo wa kifedha duniani, ambao Kihistoria, nchi za Kiafrika zimekuwa katika hali mbaya linapokuja suala la kupata ufadhili, rasilimali, na makubaliano yenye usawa ya kibiashara.
Kuzungumzia hili, nimemualika kwa njia ya simu kutoka Tanzania, Walter Nguma, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.
Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.
Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.
Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.
Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.
Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.
Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.
Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.
Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji.
Wanafanya hivyo kwa kuhamisha pesa, ujuzi, teknolojia, mifano ya utawala, maadili, na mawazo. Serikali ya Senegal inafahamu mabadiliko yanayohitajika tunapojitahidi kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulio na Utaratibu na wa Kawaida nchini Senegali.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu.
Msikilizaji, hatimaye nchi ya Tanzania imeondoa zuio ililoweka juma hili kwa ndege za shirika la Kenya KQ, uamuzi iliyokuwa imeuchukua baada ya Nairobi kukataa kutoa kibali kwa ndege za mizigo za shirika la Tanzania kushusha na kupakia kutokea Kenya.
Uamuzi huo msikilizaji ulisababisha mawaziri wa pande zote kukutana na Jumanne ya wiki hii wakakubaliana kumaliza tofauti zilizojitokeza na sasa safarai za ndege za Kenya na zile za Tanzania zitaruhusiwa.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.
Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia namna wafanyabiashara wamejipanga katika mwaka 2024, kuhakikisha biashara zao zinashamiri licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia kwa sasa.
Mwandishi wetuj Victor Moturi, kwa niaba ya mtayarishaji wa makala haya, Emmanuel Makundi, amezungumza na wafanyabiashara nchini Kenya, ambao mwaka uliopita, walilalama kupata changamoto za kifedha na hata upandaji wa bidhaa na kukosekana kwa dola.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.
Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.
From the publisher's feed
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

2 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners