
Sign up to save your podcasts
Or


Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia mkutano wa nchi ya Uchina na viongozi wa Afrika uliofanyika wiki kadhaa zilizopita, pamoja na ziara za viongozi wa nchi za Marekani, Uingereza na Ujermani kwenye nchi za Afrika Mashariki na Magharibi.
Ziara zao zinaashiria nini katika muktadha wa kiuchumi? Emmanuel Makundi amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, kuangazia haya kwa kina.
Kwenye sehemu yetu ya pili na ya mwisho kuhusu namna nchi ya Bostwana ilivyopiga hatua kwenye sekta ya madini na uchumi wake kwa kutegemea Almasi, tutasikia kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo mwekezaji binafsi Siddarth Gothi , Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo KGK Bostwana, na mchambuzi binafsi wa siasa, Marisa Lourenco, kutoka Afrika Kusini kuhusu mafanikio hayo lakini pia changamoto katika sekta hiyo.
Kati ya Oktoba 11 hadi 14 mwezi Oktoba, Bostwana iliandaa maonesho ya Kimataifa ya kibiashara jijini Gaborone, yaliyofanyika pembezoni mwa Jukwaa la kwanza wa kibiashara kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.
Bostwana ambayo uchumi wake mkubwa unategemea sekta ya madini, hasa Almasi ikiwa ya pili duniani kwa bidhaa hiyo baada ya Urusi, ilitumia fursa hiyo kujitangaza na kuvutia wawekezaji zaidi.
Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha juu kufikia 2036 kwa kupanua uchumi wake kwenye sekta nyingine kama kilimo na utalii, ni miongoni mwa mataifa duniani, ambayo taasisi za Kimataifa kama IMF na Benki ya dunia, zinasema uchumi wake unakuwa kwa kasi.
Je, Bostwana ina fursa zipi za uwekezaji hasa kwa mataifa ya Afrika Mashariki ? Wakati wa maonesho hayo, nilitembelea banda la Kenya, na leo kwenye Makala yetu ya Gurudumu la Uchumi, utamsikia Balozi wa Kenya nchini Bostwana.
Ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, unatarajiwa kupungua kasi mwaka huu, kutokana na kudorora kwa uchumi wa mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria na Angola, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia.
Ukuaji wa kikanda utapungua hadi 2.5% mwaka 2023 kutoka 3.6% mwaka jana, imesema ripoti hiyo.
Mtayarishaji amezungumza na Johnson Denge, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi, kuangazia ripoti hizi kwa kina.
Aidha kwa mujibu wa IMF Uchumi wa dunia unakua lakini sio kwa kasi, ambapo inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa dunia utapungua kutoka asilimia 3.5 mwaka 2022 hadi asilimia 3 mwaka huu na asilimia 2.9 mwaka ujao.
IMF inasema Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bei ya chakula na nishati pia unatarajiwa kupungua, ingawa polepole zaidi. Nchi nyingi zikitajwa kutokuwa na uwezekano wa kurudisha mfumuko wa bei hadi 2025.
Mwezi uliopita, viongozi wa dunia walikutana jijini New York, Marekani katika mkutano wa 78 wa baraza la umoja wa Mataifa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa dunia na ukuaji wa uchumi pamoja na mikakati ya kufikia ajenda ya mwaka 2030 na haja ya kuongeza kasi kutekeleza malengo 17 endelevu.
Kuzungumzia yaliyojiri, mtayarishaji wa makala haya alimualika Ebenezer Suleiman Mathew Ikomba, balozi wa vijana wa Tanzania kwenye umoja wa Mataifa.
Katika mijadala mingi, vijana walitajwa kuwa sehemu kubwa ya nguvu kazi ya dunia na kwamba kupitia ubunifu, uwajibikaji na harakati za kuhamasisha nchi kufikia malengo endelevu, basi dunia itakuwa sehemu salama.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia yaliyotokana kwenye mkutano huo na namna gani vijana wanaweza kushiriki katika ujenzi wa dunia salama na yenye amani ambayo itachochea maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Katika Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, mtayarishaji wa makala haya amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, ambapo wanaangazia kuhusu tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Wiki hii tunaangazia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako kunaripotiwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa madini ya shaba na kobalt katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Takwimu kutoka sekta ya madini, zinaonesha kuwa uzalishaji wa kobalt imeongezeka na kufikia zaidi ya Tani Laki moja, baada ya serikali kuwekeza asilimia 43 ya bajeti yake ya taifa kwenye sekta hiyo.
Kwenye Makala haya, mwandishi wetu wa Lubumbashi Denise Maheho, amezungumza na watafiti wa madini na mashirika ya kiraia, katika eneo la Katanga.
Serikali ya Uganda imepiga marufuku uingizwaji na uuzwaji wa nguo kukuu maarufu kama mitumba nchini humo. Rais Yoweri Museveni anasema, hatua hiyo itasaidia kukusa viwanda vya ndani vya nguo na kuunda ajira hasa kwa vijana. Mwandishi wetu wa Kampala Kenneth Lukwago anatueleza zaidi.
Athari za mabadiliko ya tabia nchi kuanzia mafuriko na ukame zimesababisha mamilioni ya raia kupoteza makazi yao, wengi wakitumbukia katika hali ya umasikini na hata kufa njaa, baadhi wakikosa huduma muhimlu ya afya, elimu huku tofauti kati ya walionacho na wasionacho ikiendelea kuongezeka, uchumi wa mataifa ukidorora.
Kwa mujibu wau moja wa Mataifa mpaka kufikia mwaka 2030 watu wanaokadiriwa kufikia milioni 700 huenda wakawa wakuhamahama kutokana na ukame peke yake.
Kuchukua hatua stahiki kukabili mabadiliko ya tabia nchi na athari zake ni jambo lisilohitaji mjadala wa muda mrefu ili kunusuru maisha ya raia pamoja na kufikia malengo endelevu ya umoja wa Mataifa.
Haya yanajiri wakati huu joto likiendelea kuongezeka, nchi zikitumia fedha nyingi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi badala ya kuwa zingeelekezwa katika kutatua changamoto za maendeleo na kiuchumi hasa kwenye nchi masikini.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaangazia ni namna gani nchi zinazoendelea zinaweza kukabiliana na athari za hali ya hewa na wakati huohuo kuwaletea wananchi maendeleo
From the publisher's feed
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

2 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners