Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Ni kufa au kupona, vita dhidi ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi barani Afrika
    Msikilizaji kwa mujibu wa tume ya maendeleo ya uchumi ya umoja wa Mataifa, kila mwaka bara la Afrika linapoteza kiasi cha dola za Marekani bilioni 88 ambayo ni sawa karibu asilimia 3.7 ya pato ghafi kutokana na biashara haramu ikiwemo utakatisha utakatishaji fedha na ukwepaji kodi.
    Makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii inaangazia suala hili kwa kina, tumezungumza na Dr Rose Mnongya, mtaalamu na mhadhiri wa uchumi katoka chuo kikuu cha St Augustine, jijini Mwanza, Tanzania.
    11 min
  • Uganda yaanza rasmi uchimbaji wa mafuta kibiashara, itanufaika vipi
    Kwa mujibu wa Serikali ya Uganda, inatarajiwa kutenegeneza mapato ya karibu dola bilioni 66 kutokana na shughuli hiyo na kiasi kingine cha dola bilioni 3 kutokana na kuchakata mafuta ghafi katika kipindi cha miaka 25 ijayo, hii ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu ya taifa hilo, kutumia rasilimali zake kujinufaisha.
    Tumezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, mtaalamu na mchambuzu wa masuala ya uchumi na umasikini akiwa nchini Tanzania, kuangazia kwa kina hatua hii ya nchi ya Uganda.
    10 min
  • Afrika na harakati ya kupunguza gharama ya usafiri wa anga, biashara
    Juma lililopita jiji la Nairobi, lilikuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi na wataalamu kutoka umoja wa Afrika na jumuiya nyingine za kikanda zaidi ya nane, ambapo walijadiliana na kukubaliana kwamba, mataifa ya Afrika lazima yatoe motisha kwa uwekezaji wa kibiashara hasa kwenye kilimo, uchumi wa buluu na mazingira ili kupunguza gharama kwa bidhaa za chakula ambazo zinaendelea kuongezeka barani Afrika.
    10 min
  • Ripoti ya Oxfam kuhusu hali ya umasikini duniani
    Msikilizaji wakati mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Uchumi duniani World Economic Forum, ukiendelea kwenye mji wa Davos, Uswis, shirika la kimataifa linalopambana na umasikini, Oxfam, linasema kwenye ripoti yake kuwa, tunaishi katika nyakati ngumu zenye kushuhudia mizozo tofauti, mamia ya watu wanakabiliwa na njaa, kupanda kwa gharama za maisha, na kwamba umasikini umasikini umeongezeka kwa kiwango cha juu katika kipindi cha miaka 25.
    10 min
  • Changamoto kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati Afrika Mashariki
    Msikilizaji kwa muda sasa, wafanyabiashara na viongozi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, wameendelea na juhudi za kujaribu kurahisisha mazingira ya kibiashara na ufanyaji biashara, kwa kuweka miundombinu itakayosaidia kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa ili kupata soko ndani na nje ya ukanda, tunaungana na Safari Fungo, mtaalamu wa biashara za kimataifa na utangamano wa kikanda, lakini pia ni mkurugenzi wa jukwaa la ubora nchini Tanzania, Nationa Quality Association of Tanzania.
    10 min
  • Maonesho ya teknolojia ya michezo ya kidijiti 'Video games'
    Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, inaangazia maonesho ya teknolojia kwa wabunifu wa michezo ya Kidijiti "Video Games", yatakayofanyika mwishoni mwa juma hili, mtayarishaji amezungumza na Douglas Ogeto, CEO wa Ludiqueworks ya nchini Kenya pamoja na Ann Ndanu, mmoja ya waandaji wa maonesho ya NAICCON 2022.
    10 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners