Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

By RFI KiswahiliBusiness
Download on the App Store

Gurudumu la Uchumi episodes

  • Ujuzi kwa vijana na teknolojia
    Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaangazia siku ya "ujuzi kwa vijana duniani' inayoadhimishwa kila tarehe 15 ya mwezi Julai kila mwaka, lengo ni kuwawezesha walimu, wakufunzi na vijana kutumia ujuzi wao kwa maendeleo.
    Leo mtayarishaji amezungumza na Tukupala Mwalyolo, msichana anayeunda ndege zisizo na rubani 'drone', pamoja na Emmanuel Cosmas Msoka, kijana mbunifu wote wakitumia teknolojia kutafuta suluhu na wako Tanzania.
    11 min
  • Faida ya mfumo wa malipo ya pamoja barani Afrika
    Mwezi Januari mwaka 2022, benki kuu pamoja na wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, waliunga mkono mchakato ulioanzishwa na benki ya Afrexim, ambayo ilitengeneza mfumo wa malipo uliolenga kurahisisha ufanyaji wa malipo na manunuzi kati ya nchi na nchi, mtu na mtu na biashara kwa biashara barani Afrika.
    10 min
  • Umuhimu wa bara la Afrika kuwa na mfumo wa pamoja wa kufanya malipo kidijiti
    Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, malipo ya kidijiti au ya kimtandao yanachangia pakubwa katika kujenga msingi imara wa kufikia maendeleo endelevu, kwanini? Ni kwasababu malipo haya yanapokuwa rahisi, salama, ya wazi na binafsi, yatawezesha ukuaji wa fursa kama nishati, maji na mikopo.
    Katika kipindi hiki utamsikia, Lucy Nshuti Mbabazi, kutoka taasisi ya umoja wa Mataifa ya muungano wa Better than Cash, Lacina Kone, mkurugenzi wa Smartafrica pamoja na Kwizela Aristide Basebya, mtafiti wa Teknolojia za Mawasiliano ya Umma na Matumizi yake serikalini, akiwa Beijing, China.
    10 min
  • SmartAfrica: Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo - Sehemu ya Pili
    Msikilizaji mataifa mengi ya Afrika, sasa hivi yanafanya juhudi kuhakikisha raia wake wanaunganishwa na huduma ya internet, kama moja ya harakati za kuchochea maendeleo kupitia teknolojia.
    Lakini kwa wananchi kuunganishwa na huduma hiyo ni jambo moja, changamoto iliyoko sasa hivi kwa nchi nyingi za Afrika ni kukosekana kwa miundombinu sahihi  kuwezesha hilo.
    11 min
  • Smart Afrika:Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo - Sehemu ya Kwanza
    Matumizi salama ya mtandao kwa maendeleo, ni moja ya ajenda iliyojadiliwa kwa kina katika mkutano wa juma lililopita nchini Zimbabwe, kuhusu namna bara la Afrika linaweza kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano, TEHAMA, kubadili uchumi wake na kurahisisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi wa bara hilo kama vile afya na kilimo.
    11 min
  • Miaka 2 madarakani ya Rais wa Tanzania
    Wataalamu wa uchumi na diplomasia wanasema, katika muda mchache aliokuwa madarakani, ameonesha dhamira ya kutekeleza mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini Tanzania, mbali na uchumi, ameshughulikia masuala ya kisiasa na kusaka maridhiano ya kitaifa, wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunaangazia miaka miwili madarakani ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
    11 min
  • Siku ya wanawake duniani na ushiriki katika ngazi za maamuzi
    Msikilizaji hebu fikiria kuwa na dunia yenye usawa. Dunia huru ya bila upendeleo na ubaguzi. Dunia jumuishi, yenye kutoa haki na shirikishi. Dunia ambayo licha ya tofauti zetu lakini bado tunaheshimiana na kufurahia. Na leo hii wataalamu wanatuambia tunaweza kusimama pamoja kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa wote bila ubaguzi wa wanawake.
    11 min

About Gurudumu la Uchumi

From the publisher's feed

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.…

More shows like Gurudumu la Uchumi

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners