Learn Swahili with SwahiliPod101!
Don't forget to stop by SwahiliPod101.com for more great Swahili Language Learning Resources!
-------Lesson Dialog-------
----Formal ----
Polisi: Je, ulikuwa pahali pa ajali, ajali ilipotokea?
Victor: Ndio, nilikuwa nimesimama barabarani nikingojea kuvuka.
Polisi: Tueleze kilichotokea kwa ufupi.
Victor: Nakumbuka kumwona mvulana mdogo kwa sketibodi lakini alipotea kwa ghafla.
Polisi: Unafahamu alikoenda?
Victor: Alianguka na kuteleza chini ya gari lililokuwa linaendeshwa.
Polisi: Je, dereva alisimama?
Victor: Alisimama kwa gutuko mkubwa. Nilikimbia kuchunguza mvulana yule.
Polisi: Hali yake ilikuwa vipi?
Victor: Alikuwa analia huku akijaribu kujivuta kutoka chini ya gari. Ambulensi ilimpeleka hospitalini.
Polisi: Habari njema. Asante kwa wakati wako.
----Formal English----
Police: Were you at the accident scene when it happened?
Victor: Yes, I was standing by the road waiting to cross.
Police: Briefly, tell us what happened.
Victor: I remember seeing a little boy on a skateboard, but he suddenly disappeared.
Police: Do you know where he went?
Victor: He fell and slid under a moving car!
Police: Did the driver stop?
Victor: He did with a loud screech. I ran to check on the boy.
Police: How was he?
Victor: He was crying while trying to pull himself out from under the car! An ambulance rushed him to the hospital.
Police: Good to hear. Thank you for your time.
---------------------------
Learn Swahili with SwahiliPod101!
Don't forget to stop by SwahiliPod101.com for more great Swahili Language Learning Resources!