Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Erasto Mwanasindele kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramihio, iliyopo Jimbo kuu la Songea swali la msikilizaji linalojibiwa linasema tukisoma katika Maandiko Mtakatifu Kitabu cha Kutoka 2o;13 imeandika usiue, Je, kwa kuua mnyama na kumfanya kuwa kitoweo ni dhambi?