Siasa na Gumzo

Siasa na Gumzo

By Standard MediaHistory
Download on the App Store

Siasa na Gumzo episodes

  • Siasa na Gumzo: Jubilee yafufuka? OKA nayo yapata marafiki wapya
    Baada ya kimya kingi na fukuzafukuza chamani, hatimaye Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na viongozi wa Jubilee katika Ikulu. Ikumbukwe chama hicho kimepanga Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe, NDC tarehe 25 Februari, 2022 katika Ukumbi wa KICC, mjadala ukiwa kuwafurusha rasmi Ruto na wandani wake kutoka chama hicho, mpango wa kushirikiana na miungano mingine na kumfanyia kampeni Raila Odinga.
    Vilevile mjadala mkali umechacha kuhusu mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi. Wana-OKA nao baada ya pigo la kondokewa na Musalia Mudavadi na Moses Wetangula imewapata washirika wengine wawili.
    Je, ni muungano gani una ufuasi makubwa? Kwa masuala na maswali haya, wanahabari wetu Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, Faith Kutere wa Uasin Gishu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wamewashirikisha wakazi katika gumzo wiki hii.
    11 min
  • Ukweli wa Mambo: Mudavadi alisema ukweli Bomas ama la? Tunaweka paruwanja
    Katika Ukweli wa Mambo leo, tunaangazia hotuba ya Musalia Mudavadi wakati Kongamano la Kitaifa la ANC, Januari 23 mwaka wa 2022. Je, aliyoyasema yana ukweli ama la na kwa kiwango gani? Huu hapa ukweli wa mambo baada ya utafiti wa kina baina ya Shirika la Habari la Standard kwa ushirikiano na kampuni ya Africa Check. Katika hotuba yake ya kipekee ya kukubali uteuzi wa kupeperusha bendera ya urais kupitia chama chake, Musalia aliahidi kufufua uchumi jinsi alivyofanya alipokuwa Waziri wa Fedha miaka ya 90. Geoffrey Mung’ou anasimulia.
    13 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; Tutarajie miungano gani baada ya Mudavadi kuungana na Ruto? Wakenya wajadili.
    Mjadala mkali umetawala vinywa vya wengi wiki hii, kufuatia hatua ya Mudavadi na Wetangula kujiondoa katika OKA na kuungana na Ruto.
    Hatua hiyo imechochea gumzo huku wengi wakijiuliza je, Ruto atavuna kura nyingi za Magharibi dhidi ya Raila?
    Hatima ya Kalonzo katika OKA ni gani hasa? Atawania urais, ama ataungana na Raila katika Azimio la Umoja?
    Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanaangazia makala hapa.
    13 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; Mudavadi awazuia Odinga na Ruto kuhudhuria NDC
    Earthquake aliyoahidi Musalia Mudavadi inasubiriwa kwa hamu kuu Jumapili. Amewaalika wana'OKA na kuwafungia nje Ruto na Raila. Wakenya wana maoni gani?
    Aidha, cheche baina ya Raila na Ruto zimezidi, kuhusu urushaji mawe na kuitana majina. Haya yanahatarisha utangamano nchini? UDA tayari imeandikia ICC ikidai serikali inafadhili vurugu kwa manufaa ya Raila.
    Vilevile tunaangazia kesi ya BBI katika Mahakama ya Juu. Je, reggae itarejea? Kadhalika tunazamia suala la mili katika Mto Yala.
    Wanahabari wetu Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, William Omasire wa Nyamira na John Mbuthia wa Nyeri wanatupambia makala haya
    11 min
  • Mwanajeshi mstaafu Marekani, anawania ubunge Marakwet Magharibi-Benson Cheserek
    Benson Cheserek ni miongoni mwa Wakenya ambao wanaishi ughaibuni (Kenyans in diaspora) na sasa analenga kuwania kiti cha ubunge kwenye eneo la Marakwet Magharibi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
    Cheserek amekuwa akiishi Marekani kwa miaka 17 ambapo amefanya kazi katika jeshi la Marekani kwa miaka 8 kabla ya kuanza biashara yake binafsi.
    Kwenye mahojiano na mwanahabari Faith Kutere, Cheserek anasema analenga kutumia ujuzi wake katika idara ya usalama kusaidia kukabili ukosefu wa usalama kwenye Bonde la Kerio, kubadili maisha ya wakazi wa eneo la Marakwet Magharibi kupitia masomo miongoni mwa masuala mengine.
    16 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: UDA yadai kwamba kamatakama ya wanaohusishwa na chuki inawalenga wanachama wake, kunani? OKA nayo yaonekana kuchanganyikiwa kuhusu siku ya kumtangaza mgombea wa urais,
    Wanasiasa kadhaa wamekamatwa kwa kuhusishwa na matamshi ya uchochezi. Swali ni je, kuna mapendeleo jinsi UDA inavyodai? Je, ni kamatakamata kwa kigezo cha mirengo ili kuleta usawa wa kisiasa?
    Aidha, Rais Kenyatta alifanya mkutano katika Ikulu na viongozi wanaounga mkono Azimio la Umoja akiwamo Raila ambapo wote walipigia debe Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa.
    Vigogo wa OKA walisusia mkutano huo wa Ikulu, licha ya kualikwa. Je, hatua yao inatoa picha gani?Vilevile, inadaiwa kwamba huenda Mudavadi akajiunga na Ruto, na Kalonzo kujiunga na Raila. Ikitokea hivyo, utapande gani utakuwa na nguvu?
    Masuala haya na mengine ndiyo yanayolipamba Gumzo la Maisha likiletwa kwako na wanahabari wetu, John Mbuthia akiwa Nyeri, Rose Mukonyo wa Machakos na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi.
    24 min
  • Kitendawili cha idadi kubwa ya wabunge kati ya mirengo ya Raila na Ruto bungeni?
    Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa umekuwa kichocheo cha mjadala wiki hii, ambapo wengi wanajiuliza iwapo kufaulu kwake kutakuwa mwanzo wa wanasiasa kuaminiana.
    Je, iwapo mswada huo utafanywa sheria, tutarajie miungano gani, hasa kati ya nani na nani?
    Na je, mswada huu umeashiria upande gani kuwa na ubabe bungeni?
    Aidha, tunaangazia mwaliko wa Ruto kwa kina Mudavadi na Wetangula licha ya kusema hawajaalikwa wala kukutana na yeyote kujadili miungano.
    Je, kuna karata gani ambayo inachezwa na wanasiasa hawa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.
    Vilevile mjadala kuhusu haja ya wanafunzi kufanyiwa vipimo vya kubaini iwapo wanatumia dawa za kulevya au la kabla ya kurejea shuleni. Je, unafikiri hatua hii itasaidia kudumisha nidhamu shuleni?
    Wanahabari wetu Faith Kutere wa Eldoret, Bernard Lusigi wa Kakamega na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wameshiriki gumzo na wananchi kuhusu masuala haya.
    12 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Mudavadi ajiunge na Raila ama Ruto?
    Mjadala mkali unaendelea kufuatia hatua ya Raila Odinga kuwatafuta marafiki wapya wa kisiasa, hasa kwenye eneo la Magharibi baada ya Mudavadi kusisitiza kwamba hatamuunga mkono tena.
    Aidha, Ruto anawataka Mudavadi na Wetangula wajiunge naye katika UDA.
    Si hayo tu, ipo hofu kutokana na kupanda kwa maambukizi ya korona hasa baada ya kugunduliwa kwa Omicron hapa Kenya.
    Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo yao kuhusu masuala haya.
    14 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Raila debeni 2022; Wana'OKA watamuunga nani?
    Tangazo la Odinga kuwania urais kwa mara ya tano, ni ithibati kamili kwamba kinyang'anyiro kitakuwa kati yake na William Ruto.
    Je, hatima ya Kalonzo, Mudavadi na Wetangula ambao walikosa kufika Kasarani ni ipi?
    Aidha, Wakfu wa Mlima Kenya Foundation, MKFumesema Raila tosha. Je, unadhani wafanyabiashara hao wataamua mwelekeo wa siasa za Mlima Kenya ama ni wananchi ndio watakaoamua jinsi anavyosisitiza William Ruto?
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo yao.
    12 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Kenya si tajiri; Wakenya wamwambia Uhuru
    Kauli ya Rais Kenyatta kuwa Kenya ni namba sita barani Afrika kwa utajiri imewaghadhabisha Wakenya wanaosema umaskini umekithiri nchini.
    Kuhusu siasa, Rais Kenyatta anasema wanasiasa viana watashindwa na wazee licha ya mbio zao za kisiasa. Je, sasa ni wazi kuwa Uhur anamuunga mkono Odinga kuwania urais? Je, hatima ya OKA ni gani? Aidha, IEBC imejiondoa katika kamati ya pamoja ya maandalizi ya uchaguzi. Maoni yako ni gani?
    Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraise wa Pokot Magharibi wametangamana na wananchi kuhusu masuala haya.
    9 min

About Siasa na Gumzo

From the publisher's feed

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.