Siasa na Gumzo

Siasa na Gumzo

By Standard MediaHistory
Download on the App Store

Siasa na Gumzo episodes

  • GUMZO LA WIKI PODCAST: Mauaji Yamezidi, Nao Wanasiasa Wamechanganyikiwa
    Suala la polisi kupewa ushauri nasaha ili kukabili msongo wa mawazo limekuwa gumzo wakati wa mazishi ya Caroline Kangogo. Ni hali ambayo imewakumba wengi. Je, lipi lifanyike ili kukabili hali hii?
    Aidha, kila kiongozi wa NASA sasa anautoroka muungano huo. Kunani? Na baada ya hatua hiyo, wataingia katika miungano gani au nani ataungana na nani?
    Raila pia amejaribu kujitangaza Mlima Kenya kupitia wanamiziki, wafanyabiashara na baadhi ya wanasiasa. Je, atabadili nyoyo za wakazi wa huko ambao wamekuwa wakimwogopa?
    Wanahabari John Mbuthia, William Omasire na Martin Ndiema wanatupambia makala haya.
    13 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST: Jubilee imesambaratika? Mpango mbadala wa BBI ni gani?
    Cheche kali za maneno zinaendelea ndani ya Jubilee baada ya kurambishwa sakafu na UDA huko Kiambaa, huku baadhi wakishinikiza kufurushwa kwa Tuju na Murathe chamani.
    Kenyatta naye amefoka akiwa Kilifi na kuwataja kuwa maadui wanaotatiza juhudi zake za kuleta umoja na maendeleo. Je, hao maadui ni akina nani?
    Vipi kuhusu reggae ya BBI? Kenyatta na Odinga wasisitiza kwamba ngoma hiyo ingalipo na kwamba marekebisho ya katiba yatafanyika. Wana njia gani mbadala ya kufanikisha lengo hilo? Huko Nyanza, tabia ya Wakenya ya kujihatarisha kwa kuchota mafuta imedhihirika tena. Je, mbona hawajifunzi kutokana na mikasa ya awali?
    Wanahabari wetu, Rose Mukonyo wa Machakos, Willie Khaemba wa Bungoma na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi na kutupambia makala ya leo.
    22 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST: Kuchanganyikiwa ndani ya NASA; Raila na Kalonzo walumbana
    Raila Odinga ameandika maono 15 ambayo angependa kuafikiwa nchini. Ruto na Mudavadi wamemsuta wakisema anashtukia mambo ambayo wengine wamekuwa wakiyazungumzia.
    Mbali na hilo, Raila anadai hakusema kwamba likuwa na risasi moja ya kuwania urais. Pia akiulizwa, anasema hajatangaza iwapo atawania. Je, unamwamini?
    Raila pia anasema kura ya maamuzi lazima ifanyike, hata miezi 3 kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.
    Suala jingine ni hatua ya Uhuru kuzindua usiku huduma za afya Nairobi, huku akieleka Ukambani mchana kuzindua miradi. Mbona asizindue miradi yote usiku ikizingatiwa kuwa korona ingalipo?
    Kwa uhondo kamili kuhusu masuala haya, wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo hayo.
    13 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST: Wakenya kuhusu BBI, mikopo na utapeli wa wabunge
    Mapambano ya kisheria yamedhihirika katika Mahakama ya Rufaa. Hoja kuu ikiwa mwasisi hasa wa BBI ni nani. Ni Rais Kenyatta, Raila Odinga au ni Junet Mohammed na Dennis Waweru? Aidha, ripoti ya Mhasibu Mkuu wa Serikali imeweka wazi jinsi wabunge wanavyopora pesa za umma kupitia marupurupu ya usafiri.
    Pia, serikali inaendeleza kopakopa na mara hii Rais amekwenda kuomba bilioni 160 nchini Ufaransa huku serikali ikikosa kutii agizo la IMF kwamba ichapishe majina ya Covid-19 billionairs. Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, said Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.
    17 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST; Uhuru asema atamuunga mgombea wa NASA; hoja za Wakenya
    Suala la viongozi wote kutakiwa kuwa na digrii ili kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa limezua gumzo nchini huku Naibu wa Rais, William Ruto akiungana na wanaopinga hitaji hilo lililotajwa na IEBC.
    Tayari Seneta Kipchumba Murkomen ameandaa mswada unaolenga kufutilia mbali hitaji hilo huku watakaowania wakitakiwa kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika lugha za Kiswahili na Kiingereza pekee na wenye mahitaji maalumu kujua lugha ya ishara.
    Je, uongozi unategemea kiwango cha masomo?
    Aidha, Rais Kenyatta amesema yu tayari kumuunga mkono mgombea wa NASA suala ambalo limempandisha hasira Ruto. Isitoshe, Kalonzo ameapa kutokuwa mgombea mwenza wa Raila, huku akiambiwa aache kubweka.
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wamewashirikisha Wakenya katika gumzo. hili.
    13 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Wakenya wakosoa bajeti; haimjali mtu wa kawaida
    Hisia kali zimejitokeza kufuatia bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha, Ukur Yattani huku Wakenya wakilalamikia kukandamizwa kwani watazidi kutozwa kodi ya juu ili kufadhili bajeti hiyo ya shilingi trilioni 3.6.
    Wakulima nao wanalalamikia kukandamizwa kwa sekta ya kilimo ilhali ni uti wa mgongo wa taifa hili.
    Vilevile, Wakenya wameghadhabishwa na kauli ya Waziri Yattani kwamba serikali itaendelea kukopa kwani watatozwa kodi zaidi. Aidha, mashinikizo yanazidi kutolewa kwa Rais Kenyatta kuwaapisha majaji sita ambao aliwaacha nje wakati wa uteuzi wake.
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Faith Kutere wa Uasin Gishu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
    16 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST; Rais anahujumu idara ya mahakama, Wakenya wazungumza
    Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kuwaidhinisha majaji 34 na kuwaacha 6 akiwamo, Joel Ngugi na George Odunga ambao walikuwa miongoni mwa majaji walioharamisha BBI, imeendelea kuibua hisia kinzani hasa kuhusu uhuru wa Idara ya Mahakama. Je, unadhani Rais analipiza kisasi ama kuna sababu maalumu za kuwakataa sita hao?
    Aidha, katika maadhimisho ya Madaraka, Rais aliendelea kushtumu mahakama akisema majaji wanatoa uamuzi bila kujali athari zake kiuchumi. Je, unafikiri majaji wanatumia sheria kuhujumu serikali ama ni serikali ndiyo inayokiuka katiba?
    Si hayo tu, Rais Kenyatta amekosolewa vikali baada ya kuzindua miradi kwenye eneo la Nyanza. Je, anafanya maendeleo kwa ubaguzi?
    Wanahabari wetu Moses Kiraise wa Pokot Magharibi, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wananchi kuhusu masuala haya.
    15 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST; BBI iendelee au la? Uhuru ataacha rekodi ya maendeleo? Wakenya wanajadili
    Mjadala mkali unaendelea kuhusu iwapo mchakato wa BBI unafaa kusitishwa kabisa hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao au la. Naye Naibu wa Rais, William Ruto amesema kusimamishwa kwa BBI mahakamani vilevile mikutano ya kisiasa ni ujumbe kwamba pana haja ya mashauriano kufanyika kuhusu mustakabali wa Kenya.
    Aidha, Kenyatta amezindua upya Kiwanda cha Nyama, KMC chini ya Jeshi la Ulinzi KDF, akisema anategemea sana KDF katika kutekeleza maendeleo kwa sababu ya bidii, uwajibikaji na bajeti yake nafuu ikilinganishwa na zile za wanakandarasi wengine.
    Je, Rais Kenyata ataacha rekodi gani ya uongozi ikizingatiwa kwamba mahakama imekuwa ikitoa maamuzi ya kuharamisha mipango yake ukiwamo uhamisho wa KMC kutoka Wizara ya Kilimo hadi KDF?
    Wanahabari wetu, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi, Robert Menza wa Mombasa na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wananchi katika makala haya.
    13 min
  • GUMZO LA WIKI PODCAST: Kivumbi cha chaguzi ndogo, vilevile BBI; Wakenya wanasemaje?
    Wakenya wanatoa hisia kali kuhusu chaguzi ndogo za Bonchari, Juja na Rurii ambapo polisi wengi walionekana, suala ambalo wengi hata viongozi walilalamikia vikali. Aidha, kung'aa kwa UDA na kushindwa kwa Jubilee katika chaguzi ndogo kumechochea mjadala nchini. Jambo jingine ni je, Mahakama ya Rufaa pia itaangusha BBI au la? John Mbuthia wa Nyeri, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
    13 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; Kweli, twachangia mimba na kuvunja ndoa - waendesha bodaboda wakiri
    Kufuatia madai mengi kwamba waendesha-bobaboda wanaongoza katika kushiriki mapenzi na wasichana pia wanawake walioolewa, tumezungumza na baadhi yao kujua kama ni kweli, vilevile kulenga kujua sababu. Wanakiri, huku wakisema wanawake wenyewe ndio huwatongoza. Mmoja wao anakiri kujihusisha na zaidi ya wanawake 80. Sikiliza mazungumzo baina yao na wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Willie Khaemba wa Bungoma na Martin Ndiema wa Kitale.
    25 min

About Siasa na Gumzo

From the publisher's feed

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.