Siasa na Gumzo

Siasa na Gumzo

By Standard MediaHistory
Download on the App Store

Siasa na Gumzo episodes

  • Gumzo la Wiki Podcast: Mawe Kondele; Ruto alaumiwa
    Naibu wa Rais William Ruto abebeshwa lawama kuhusu vuruga za Kondele. Je, vuruguzu hizo zilichochewa kisiasa anavyodai?
    Na je, Ruto alifanya makosa kumshtumu Odinga katika ngome yake?
    Adha, Wakenya wanahisi kwamba Kalonzo Musyoka amekosa mwelekeo na wakati umefika kwake kutangaza wazi msimamo wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
    Vilevile, Nick Mwendwa atakiwa kueleza jinsi amekuwa akiendesha shughuli za FKF.
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Washington Onyango wa Kisumu na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
    7 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; OKA yafufuka, Jubilee ikiwaka moto
    Imekuwa wiki yenye matukio kadhaa ya kisiasa huku muungano wa OKA ulioonekana kufifia ukifufuka kwa mikutano ya kuwatia wasiwasi wapinzani japo swali ni lile lile la ni nani atakayepata tikiti?
    Kule Jubilee, mikakati ya kumtema Ruto rasmi inaendelea huku naye akiendeleza cheche kali, wakati huu akikosoa mikopo waliyoichukua kwa pamoja na Rais Kenyatta. Wanafunzi nao wamefanikiwa kuishinikiza serikali kuwapa likizo. Ndiyo suluhu ya mioto shuleni?
    Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia sehemu hii.
    21 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Waiguru ahamia UDA; OKA yapinga kugawika
    Gavana wa Kirinyaga, Ann Waiguru aigura Jubilee na kujiunga na UDA. Je, Ruto atamchagua kuwa mgombea mwenza?
    Je, ataweza kumenyana na Purity Ngurici na Martha Karua?
    Vilevile, Wakenya wamkumbusha Kenyatta ahadi ya kutoa mwanga zaidi kuhusu ufichuzi wa Pandora Papers.
    Aidha, Mudavadi na Kalonzo watakiwa kuweka wazi misimamo yao kuhusu kinyang'anyiro cha urais mwaka ujao. Watakwenda hadi debeni au la?
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshirika gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
    15 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; Kafyu na vicheko vya UhuRuto; maoni ya Wakenya
    Kuondolewa kwa marufuku ya kuwa nje kwashabikiwa na Wakenya. Aidha, Mt. Kenya yasubiri ahadi ya Uhuru kuhusu kilichomkosanisha yeye na Ruto. Huko Kisii, hulka ya kuwateketeza wazee kwa madai ya kushukiwa kuwa wachawi yazua ghadhabu na kauli kinzani. Wanahabari wetu, John Mbuthia, William Omasire na Martin Ndiema wamewashirikisha wananchi kuhusu haya.
    11 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Mt. Kenya Foundation ina ushawishi wa kisiasa?
    Vikao vya Wafanyabiashara wa Mount Kenya Foundation vimetikisa siasa za Kenya wiki hii, baada ya kusema wataamua kuhusu mgombea wa urais watakayemuunga mkono miongoni mwa vigogo wa OKA na Raila.
    Je, ajenda ya wafanyabiashara hao ni kumkabili Naibu wa Rais, William Ruto au ni kupigania maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya?
    Aidha, ufichuzi wa Pandora Papers umeibua maswali mengi kuhusu uzalendo wa Kenyatta na uhalali wa mali fiche na akaunti zake za siri nje ya Kenya.
    Je, ufichuzi huo utasaidia kukabili ufisadi nchini?
    Na je, Wakenya wanahisi vipi kuhusu matokeo duni ya Timu ya Taifa ya Harambee Stars?
    Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki Gumzo na wakazi wa maeneo yao kuhusu masuala haya.
    17 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; Gideon Moi debeni 2022; hofu UDA na OKA
    Kuidhinishwa kwa Gideon Moi kupeperushwa bendera ya KANU kumezidisha ushindani wa urais kuelekea 2022. Aidha, Rais Kenyatta anawawinda wana-OKA usiku na mchana ili wote waseme Mzee Tinga tosha. Na je, wabunge wa Kieleweke watafaulu kumfanyia Odinga kampeni Mlima Kenya? Nao wandani wa Ruto wanasema wafanyabiashara wa Mt. Kenya Foundation hawana usemi wa kisiasa.
    Vilevile tumeangazia Mswada wa NHIF na mpango wa Afya kwa Wote, UHC?
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.
    27 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Waiguru ajongea UDA, naye Raila amlaumu Ruto kuhusu BBI
    Je, ni kweli kuwa BBI ilichangia kukwama kwa miradi ya maendeleo? Kuna haja ya Rais Kenyatta na Odinga kuwaomba Wakenya msamaha kwa kuhujumu maendeleo kupitia BBI jinsi anavyodai Naibu wa Rais, William Ruto? Na je, ni sawa kwa Kenyatta na Odinga kumlaumu Ruto kwa kuchangia kuanguka kwa BBI au ni visingizio tu?
    Aidha, siasa za eneo la Kati zinazidi kuwa ngumu, Martha Karua akiteuliwa kuwa Msemaji wa Mt. Kenya Unity Forum. Ataweza?
    Huko Kirinyaga, Gavana Ann Waiguru aambiwa ahamie UDA ili achaguliwe tena siku chache tu baada ya Kalonzo kumtaja kuwa mmoja wa wana'OKA.
    Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.​
    19 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Usalama Laikipia; siasa za 2022-Wakenya wazungumza
    Suala la usalama huko Laikipia linazidi kuwa kero huku wanasiasa wakilaumiwa kuchochea hali hiyo. Je, nani wa kulaumiwa kufuatia kudorora kwa usalama? Ruto naye amemjibu Matiang'i kuwa iwapo anadhani ana ardhi Laikipia, basi awagawie wakazi.
    Katika ulingo wa siasa, Mlima Kenya imekuwa kama msichana mrembo anayemezewa mate huku kila anayetaka kuwania urais akitafuta mgombea mwenza huko.
    Nani awe mgombea mwenza wa nani? Aidha, viongozi wameanza ujanja wa kuwa karibu na Mkenya huku Raila akitumia usafiri wa umma.
    Kadhalika, CBC imewafikia kooni wazazi kutokana na mazoezi ya ajabu wanayowasaidia wanao kufanya.
    Wanahabari wetu, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na John Mbuthia wa Nyeri wanatupambia makala haya.
    13 min
  • Gumzo la Wiki Podcast; Usalama wa Ruto - Wakenya wazungumza
    Suala la usalama wa Naibu wa Rais, William Ruto limezua mjadala mkali wiki hii na hata kugeuka kuwa mazungumzo ya kulinganisha mali anayomiliki Ruto dhidi ya viongozi wengine.
    Aidha, maswali mengi yameibuliwa kufuatia jinsi Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang'i alivyotumia vikao vya bunge kutangaza mali ya Ruto hasa inayolindwa na maafisa wa usalama. Je, unadhani hatua hiyo imemmaliza au ndiyo imemjenga Ruto kisiasa?
    Vilevile siasa za Mlima Kenya zinazidi kushika kasi huku baadhi ya viongozi wakisema Raila anatosha licha ya kufikirika kuachwa na Uhuru kujitafutia kura mlimani.
    Si hayo tu, Waziri wa Elimu Prof. Geoge Magoha anasema mzazi ambaye mwanawe hajaenda shuleni atakamatwa.
    Wanahabari wetu; John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraise wa Pokot Magharibi wametangamana na wananchi kupata hisia zao katika makala haya.
    13 min
  • Gumzo la Wiki Podcast: Ziara ya Ruto Uganda - cheche za ODM na NRM; kauli za Wakenya
    Suala la kuzuiwa kwa Ruto kwenda Uganda linazidi kuzua gumzo, taifa hilo likisema halikufahamu kuhusu ziara hiyo. Karanja Kibicho naye anasema ofisi yake haikuwa na habari. Nani hasa aliyepiga simu Ruto azuiwe? ODM nayo inasema Ruto alilenga kwenda Uganda kujifunza namna ya kutwaa uongozi kwa nguvu ama kukatalia madaraka.
    Je, bottom up ni ya kuinufaisha Uganda jinsi inavyodai ODM? Naye Murathe amewasisitizia Wakenya kwamba Raila ndiye atakayekuwa Rais 2022. Murathe anajua siri gani ya kufanikisha hilo? Na je, Raila atakubaliwa Mlima Kenya?
    Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wametangamana na wananchi kuhusu masuala haya.
    17 min

About Siasa na Gumzo

From the publisher's feed

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.