Mwanamuziki Kampo Mphela anasema muziki wa vuguvugu la utamaduni wa Afrika Kusini, Amapiano, unaendelea kupata umaarufu duniani na wiki hii mwandishi wetu Harrison Kamau anaangaza yale yaliojiri New York katika burudani mbalimbali kikiwemo kikundi hicho cha muziki.
Msimu wa pili wa Ligi ya mpira wa kikapu ya Afrika, BAL, imeanza huko Dakar, Senegal, huku miji mingine ya Kiafrika ambako michezo hiyo itafanyika ikiwa ni Cairo, Misri na Kigali Rwanda.
Serikali ya Tanzania imeamua kutambua kazi za sanaa na hivyo wasanii wameanza kulipwa kutokana na kazi zao, wakati tayari baadhi ya wasanii wameanza kulipwa fidia ya kazi zao.