Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha kwenye mkutano wa hivi majuzi wa CSW69 kufuatilia harakati za Mfuko wa CRDB za kujengea uwezo na kuinua wanawake nchini Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno “MHARUMA.”Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wa misaada ya kibinadamu leo wamesema wanaendelea kuwasaidia watu wa Muyanmar na mahitaji ya msingi baada ya tetemeko kubwa la ardhi la Ijuma iliyopita ambapo idadi ya waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 2,800, maelfu wamejerihiwa na mamia bado hawajulikani wako.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amesema leo kwamba ameshtushwa na ripoti za mauaji ya raia bila kufuata utaratibu wa kisheria yaliyoenea mjini Khartoum baada ya kurejeshwa kwa mji huo chini ya udhibiti wa Jeshi la Sudan (SAF) tarehe 26 Machi.Na majadiliano ya siku mbili ya kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madrid yameanza leo Nairobi Kenya mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo. shududa wetu huko ni Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MHARUMA”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!