Hii leo jaridani tunaangazia kilichojiri katika Mkutano wa COSP11 kuhusu ufisadi mjini Doha Qatar, haki za kibinadamu na vijana nchini Kenya, afya ya akili ikimulika upweke na jinsi unavyoweza kuepukana nayo.Mkutano mkubwa zaidi duniani wa kupambana na rushwa au ufisadi umeanza leo Desemba 15 mjini Doha nchini Qatar kwa wito wa kutumia teknolojia zinazoibuka katika mapambano dhidi ya rushwa na kushughulikia uhusiano wake na uhalifu wa kupangwa na makosa mengine ya kifedha.Haki ni msingi wa Kila siku, hiyo ndio ilikuwa kaulimbiu ya siku ya Haki za binadamu mwaka huu iliyoadhimishwa wiki iliyopita. Lakini kila uchao haki za binadamu zinaendelea kukiukwa kuanzia nyumbani hadi kwenye mtandao. Kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha vijana katika kupambana na ukiukwaji wa haki hasa mtandaoni, Ofisi ya Umoja wa Maataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) jijini Nairobi Kenya umewakusanya vijana kujadiliana nao na kuwapa mafunzo ya kumakinika hasa mtandaoni.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO linaendelea na mfululizo wa programu ya kuiunganisha jamii au Social Connection ikiwa na lengo la kusaidia watu kutojitenga na kujihisi wapweke, mmoja kati ya walionufaika wa programu hiyo ni Roz, binti mwenye umri wa miaka 21 raia wa India, aliyehisi upweke mkubwa wakati baba yake alipokuwa akipambana na ulevi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!