Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kajiado iliyoko Kusini na Kusini magharibi mwa jiji la Nairobi nchini Kenya kumulika upatikanaji wa huduma za choo na hasa choo safi na salama ambazo bado ni kizungumkuti kote dunianini.Katibu Mkuu wa Umoja wa, António Guterres,akizungumza na waandishi wa habari hii leo ametoa onyo kali COP30 huko Belém, Brazil, akisisitiza dharura ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Amesema “Jamii zilizo mstari wa mbele zinaangalia zikiesabu nyumba zao zilizozamishwa na mafuriko mavuno yaliyoshindikana, vyanzo vya maisha vilivyopotea na kuuliza kwa kiasi gani zaidi wateseke . Wamesikia visingizio vya kutosha, sasa wanatakahatua”.Leo ni Siku ya mtoto Duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Sikilizeni watoto, simameni kwa ajili ya haki za kila mtoto, kila siku.” Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo ya Hali ya Watoto Duniani 2025 sanjari na maadhimisho haya inaonya kwamba zaidi ya watoto milioni 417, sawa na mtoto 1 kati ya 5 katika nchi za kipato cha chini na cha kati, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji muhimu angalau katika maeneo mawili ya msingi ya maisha.Mkutano wa wanaharakati vijana wavumbuzi kutoka kila pembe ya dunia umeaanza leo mjini Geneva Uswisi ukibeba mafda kuu “Kutoka Hashtag hadi Hatua”, ukisherehekea vijana wanaobadilisha maisha ya jamii zao kupitia zana za kidijitali na majukwaa ya mtandaoni. Mwaka huu, washindi wa uvumbuzi huo wanatoka nchi mbalimbali, ikiwemo Côte d’Ivoire, India, Lebanon, Japan, na Brazil, wakitambuliwa kwa kazi zao zenye athari kubwa chanya. Waandaaji wa Jukwaa hilo amba oni Umoja wa Mataifa wanasema tukio hili lina lengo la kuhamasisha vijana wengi zaidi kubadilisha ushiriki wao wa mtandaoni kuwa hatua halisi zinazoboresha jamii, kuthibitisha kuwa uanaharakati wa kidijitali unaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Na katka kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MTAWALIA.”Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!