Hii leo jaridani tunaangazia usafirir endelevu, udhalilishaji wa mtandaoni tukikuletea ujumbe kutoka Uganda, na ufugaji endelevu unaowawezesha wafugaji katika maeneo kame ya Isiolo na Garissa nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri Endelevu Duniani kwa kuonya kwamba mifumo ya usafiri duniani ambayo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya kila siku inayochochea dunia kuelekea janga la tabianchi na kwa hivyo siku hii inatukumbusha kwamba njia ya kuelekea mustakabali bora inategemea mifumo safi na yenye uendelevu wa usafiri.Siku 16 za uhamasishaji kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea leo tunakupeka mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusiki maoni kutoka kwa wa mji huo kuhusu ukatili mtandaoni yakienda sanjari na kauliimbiu ya kampeni ya ya mwaka huu isemayo “Ukatili wa mtandaoni ni ukatili halisi na hakuna visingizo kwa ukatili mtandaoni”.Katika maeneo yaliyoghubikwa na athari za mabadiliko ya tabianchi kaskazini mwa Kenya, wafugaji wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa kwani ukame na mafuriko, vinatishia sio tu mali zao bali pia maisha yao. Lakini kupitia mradi wa bima ya mifugo unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, kwa ushirikiano na asasi ya Zoetis na kampuni ya ZEP-RE, jamii zinaanza kupata ahuweni na matumaini mapya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!