Hii leo jaridani tunaangazia hali ya amani na usalama nchini Guinea-Bissau, utapiamlo nchini Sudan na juhudi za UNICEF za kuwawezesha vijana ili waweze kujikwamua kimaisha nchini Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba.Zaidi ya miaka miwili na nusu ya vita nchini Sudan imewaacha watu milioni 21 karibu nusu ya watu wote wa nchi hiyo wakikabili njaa kali, huku maeneo mawili yakithibitishwa kukumbwa na baa la njaa. Mapigano yamepungua kwa sasa katika baadhi ya sehemu za Khartoum, na masoko yanaanza kufunguliwa tena., Lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linaonya kuwa hali bado ni tete.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) kupitia programu yake ya stadi za maisha na mafunzo ya biashara iitwayo Ujana Salama, inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini humo TASAF kwa msaada wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewezesha kikundi cha vijana nchini humo kujitegemea. Mmoja wa vijana wanufaika wa programu hiyo ameweza kujenga mustakabali ambao awali aliouna kama ndoto kupitia masomo ya ushoniMwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!