Jua Haki Zako

Jua Haki Zako

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Jua Haki Zako episodes

  • DRC : Haki ya wanawake kupata elimu

    Nchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati.

    Katika makala haya basi Butua Balingane, mkurugezi wa chuo kikuu cha walimu cha ISP, Goma ambaye anasimulia masaibu anayopitia mtoto wa kike nchini DRC kupata elimu.

     

    Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

    11 min
  • Kenya : Wanawake 97 wauawa kwa kipindi cha miezi tatu

    Nchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa.

    Ni visa ambayo vimesababisa viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais William Ruto, ambaye ametoa agizo wa asasi za uchunguzi nchini humo kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika visa hivyo.

     

    Kwenya makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Kenya, ambapo mtaalamu wa maswala ya jamii bi Carolina Situma anaeleza nini kimechangia mauwaji haya.

    10 min
  • Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka

    Nchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari.

    Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.

    10 min
  • Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani

    Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia.

    Katika mwaka 2024, mada ilikuwa "Kutoa sauti kwa watoto wa kike: Fursa na Changamoto katika Utu wa Kike."

    Makala haya yataangazia kwa kina haki za mtoto wa kike na hatua zilizopigwa katika kusababisha mtoto wa kike kuskizwa na hata hatua zilizochukuliwa ili kuboresha elimu, afya, na usalama wa watoto wa kike, pamoja na jinsi jamii zinaweza kushiriki katika kuwasaidia kufikia ndoto zao.

    Aidha, itajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wazazi katika kufanikisha malengo haya.

    10 min
  • MAMILLIONI YA WATU HASA WATOTO BARANI AFRIKA HAWAJAPATA HAKI ZA CHAKULA

    Chakula ni muhimu kwa maisha, kuishi, heshima, ustawi, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa  watu binafsi, jamii, na mataifa. Sheria za kimataifa zinatambua haki ya kila mtu kupata chakula cha kutosha na haki ya kuwa huru kutokana na njaa. Haki hii ni ya msingi kwa utekelezaji wa haki zote za binadamu.

     

    Nchini  Kenya, ni haki ya kikatiba, iliyoko  katika Kifungu cha 43(1)(C) kinachosema: "Kila mtu ana haki ya kuwa huru kutokana na njaa na kuwa na chakula  bora na cha kutosha .Lakini je, sheria hii inatambuliwa ? Je, watu wanaelewa haki yao ya chakula? Na hali ya usalama wa chakula nchini Kenya iko vipi leo?

    Katika kipindi cha leo ,cha jua haki zako , tunaangazia iwapo watu wanapata haki zao za kupata  chakula na jinsi changamoto za kiuchumi na kimazingira zinavyoathiri upatikanaji wa chakula nchini Kenya

    10 min
  • DRC : Wanawake wabakwa katika gereza la Makala nchini

    Katika makala haya tunaangazia ripoti ya umoja wa mataifa kusema kwamba zaidi ya wanawake wafungwa ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela.

    Ripoti hiyo imebaini kwamba kati ya wafungwa 348 katika gereza hilo la Makala, wafungwa 268, walitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ubakaji,  wanawake 17 kati ya waliobakwa wakiwa chini ya umri wa miaka 19.

    Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.

    Awali serikali ya DRC ilikuwa imekiri kubakwa kwa wanawake hao ila haikotoa idadi ya wanawake waliobakwa.

    Kadhalika ripoti hiyo pia imesema wafungwa 129 waliojaribu kutoroka jela waliuawa kwa kupingwa risasi, katika gereza hilo la Makala ambao linastahili kutoa huduma kwa wafungwa 1500, ila lina zaidi ya wafungwa alfu 15.

    Rais Felix Tshisekedi aliagiza kufanyika kwa uchuguzi kuhusiana na jaribio hilo la wafungwa kutoka, na mikakati ya kupunguza idadi ya wafungwa katika gereza hilo la jiji Kinshasa.

    10 min
  • Kenya : Watoto wateketea shuleni, je jukumu la nani kumlinda mtoto akiwa shuleni

    Nchini Kenya zaidi serikali inaendesha uchunguzi wa chembechembe za DNA, za wanafunzi 21 wa shule ya msingi ya Endatasha baada yao kuteketea kiasi ya kutotambulika, kabla ya miili yao kutolewa kwa familia.

    Miili limewaacha wazazi kwenye njia panda wasijue la kufanya, wakati huu maswali yakiendelea kuulizwa je nani wakulaumiwa baada ya mkasa huo wa moto shuleni.

     

    Kufahamu mengi skiza makala haya.

    10 min
  • Kenya: Vikundi vya kina mama vyajitokeza kupinga ukeketaji

    Katika makala haya tunajikiti kuangazia uketetetaji ambapo wasichana  wamekuwa ukiendelea kukeketewa nchini Kenya licha ya serikali kanzisha kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu athari zinazotokana na ukeketaji huo.

    Jamii za Kenya, kupitia kwa kina mama na wasichana waliopitia ukeketaji  kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii wameanzisha vikundi vya kutetea haki za wasichana ili kuwalinda kutokana na ukeketaji huo.

     

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    11 min

About Jua Haki Zako

From the publisher's feed

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

More shows like Jua Haki Zako

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

1 Listeners