
Sign up to save your podcasts
Or


Serikali ya Uganda inapata shinikizo kutoka kwa wapinzani na watetezi wa haki za binadamu kumwachia huru mwanasiasa mkongwe Kizza Besigye anayekabiliwa na mashaka katika Mahakama ya kijeshi ambaye kwa siku kadhaa sasa amegoma kula akiwa gerezani, hali ambayo imedhoofisha afya yake.Tulimuuliza msikilizaji anazungumzia vipi masaibu yanayomkumba Besigye na anafikiri ni kwanini inachukua muda kuihamisha kesi ya mwanasiasa huyo kutoka Mahakama ya kijeshi kwenda kwenye Mahakama za kiraia ?
Katika makala haya tunazama kuangazia hali ya kibinadamu kule Goma baada ya waasi wa M23 kuwasili katika mji huo.
Je hali ya kibinadamu ipo je baada ya waasi wa M23 kuwasili Goma.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limechapisha taarifa lituhumu serikali za Africa namna gani zimeshindwa kulinda haki za raia wake.
Katika makala haya Benson Wakoli amezungumza na maafisa kutoka Human Right Watck kuelewa hali kamili/.
Skiza makala haya kuelewa zaidi.
Katika nchi nyingi barani Afrika, adhabu ya kifo inasalia kuwa suala tata, ikiwa imejikita katika mifumo ya kisheria na kijamii. Licha ya mjadala kuhusu ufanisi na maadili yake kuendelea, wanaharakati wa haki za binadamu wanajitahidi kuhakikisha kufutwa kwa adhabu hiyo, wakisisitiza haki ya msingi ya kuishi. Ulaya tayari imeondoa adhabu ya kifo, ikitoa mfano wa mfumo wa haki unaolenga marekebisho badala ya adhabu kali.Kwenye makala haya tumeangazia juhudi hizo kuondoa adhabu hiyo .
Siku ya Jumatatu asubuhi Vijana wanne kati ya 6 waliotekwa nyara katika wiki za hivi majuzi waliachiliwa huru, saa chache kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika kupinga kutoweka kwao.
Billy Munyiri Mwangi na Peter Muteti waliungana na familia zao huko Embu na Nairobi, mtawalia, baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili ilhali Rony Kiplangat alipatikana katika kaunti ya Machakos naye Benard Kavuli akapatikana katika maeneo ya Kitale magaribi mwa nchi.
Katika makala Jua haki zako, tunaangazia huru wa kutumia mitandao ya kijamii na katika kutumia mitaoa hiyo kuna mipaka yake. Je nchini Kenya hatua zipi zinafaa kuchukuliwa ikiwa mshukiwa atapatikana na hatia ya kukiuka huru ywa mitandao ya kijamii.
Makala jua haki zako leo yataangazia haki za kina dada,changamoto wanazopitia na nini wanaharakati wanafanya ili kuhakikisha visa vya dhulma vinaripotiwa kwa wakati na haki inatendeka.
Kumbuka killa mwaka, kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba, dunia inaungana kwa pamoja kutambua changamoto kubwa zinazowakumba wanawake na wasichana, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, ukatili wa kifamilia, na vitendo vingine vyote vya ubaguzi na dhuluma.
Joy Zawadi, mkurugezi mkuu wa shirika la Akili Dada, linalopigania haki za mtoto wa kike alikiti chini na Benson Wakoli, kujadili juhudi wanazofanya kuinua mtoto wa kike nchini Kenya.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Haya ni awamu ya pili ya makala haya, ambapo Joy Zawadi afisa Mtendaji kutoka shirika la Akili Dada, anaendelea kujadili namna gani haki za mtoto wa kike zinaweza kuheshimiwa.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Moses Balagisi, afisi kutoka shirika la umoja wa Africa linaloshirikiana na masharika ya kiraia, kuhakikisha uongozi wa juu wa AU unaskiza kilio cha raia wa chini, analeza namna gani wanahakikisha hilo linafanyika.
Kufahamu mengi zaidi, skiza makala haya.
Wahudumu wa afya nchini Kenya wanaitaka serikali kuwatuma kazini wanafunzi na wahudumu wa afya mara moja na kufuta malimbikizo ya mishahara ya madaktari kulingana na Makubaliano ya Pamoja ya 2017.
Wahudumu wa afya ambao wamehudumu kwa miaka minne chini ya kandarasi katika taasisi za afya ya umma wanadai ajira ya kudumu ambayo walikuwa wamehakikishiwa na serikali ya Kenya kufuatia miaka mitatu ya huduma.
From the publisher's feed
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

2 Listeners

0 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

1 Listeners