Jua Haki Zako

Jua Haki Zako

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Jua Haki Zako episodes

  • Kenya : Sanaa ya wanafunzi wa shule yakera serikali

    Mjadala makali bado unaendelea baada ya serikali kudaiwa kuzuia wanafunzi wa shule ya upili ya Butere kuwasilisha uchezo wao wa Echoas of War kwenye ngazi ya kitaifa kwenye mashindao ya kuingiza.

    Kisa na maana ni kwamba mchezo huo unaikosoa serikali na kwamba uliandikwa na mwanasiasa ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha UDA, Bwana Cleophas Malala. Kauli ya wanafunzi kupitia mchezo wa kuigiza wa "Echoes of Doom" imeibua maswali mazito kuhusu uhuru wa kujieleza, demokrasia na usalama wa taifa.

    Wanafunzi hawa walitumia jukwaa la sanaa kuelezea hali  halisi ya jamii, lakini kile kilichoanza kama onyesho la kisanaa , limeibua hisia mseto baada ya madai kwamba serikali iliwazuia wanafunzi hao kuonyesha sana hiyo kwenye ngazi ya kitaifa.

     

    Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

    10 min
  • Haki ya maakazi bora kwa jamii zetu

    Katika makala haya tunajadili haki ya raia kuwa maakazi bora ambapo maelfu ya wazee, walemavu, na wajane nchini Kenya wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa za makazi duni, hasa katika maeneo kame na mitaa duni.

    Hali hii imewalazimu wengi kuishi katika mazingira yasiyofaa, huku baadhi yao wakikosa makazi kabisa.

     Hata hivyo, kwa ushirikiano wa wahisani, mashirika ya kijamii, na serikali za kaunti, mpango wa kuwajengea makazi bora umeanzishwa katika kaunti mbalimbali, ukiwapa matumaini wapate hifadhi salama na yenye hadhi.

    Katika kijiji cha Naibor, Kaunti ya Laikipia, baadhi ya wazee tayari wameanza kunufaika na mpango huu.

     

    Skiza maka haya kufahamu mengi

    10 min
  • Wazee na Wasiojiweza wafaidika na Mpango wa Makazi Bora Nchini Kenya

    Maelfu ya wazee, walemavu, na wajane nchini Kenya wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa za makazi duni, hasa katika maeneo kame. Hali hii imewalazimu wengi kuishi katika mazingira yasiyofaa, huku baadhi yao wakikosa makazi kabisa. Hata hivyo, mpango wa kuwajengea makazi bora umeanzishwa katika kaunti mbalimbali, ukiwapa matumaini wapate hifadhi salama na yenye hadhi. Katika kijiji cha Naibor, Kaunti ya Laikipia, baadhi ya wazee tayari wameanza kunufaika na mpango huu.

    10 min
  • Tamaduni na sheria zetu wapi Mipaka ?

    Kwenye makala haya  tunajikita na kuzama kuangazia tafauti iliopo kati ya haki, sheria na dhuluma dhidi ya wanawake.

    Haya yote ni kutoka na familia moja nchini Kenya eneo la Narok, ambayo  inalilia haki baada ya msichana wao kutetendwa vitendo vya kinyama kutokana tamaduni za jamii ya Kisii kumtaka amwange mchanga ndani ya kaburi la aliyekuwa bwana yake kinyume na matakwa yake.

    Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

    10 min
  • Machi nane siku ya kuangazia haki za mwanamke

     Kwenye makala haya tunaangazia Siku ya kimataifa ya wanawake, inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,  siku hii hutumika kutambua mchango wa wanawake katika jamii na kupigania usawa wa kijinsia.

    Ni siku ya kusherehekea mafanikio ya wanawake katika nyanja mbalimbali kama vile siasa, uchumi, sayansi, na sanaa, huku ikihamasisha juhudi za kuondoa changamoto wanazowakabili wanawake, kama vile ubaguzi, ukatili wa kijinsia, na ukosefu wa fursa sawa.

    Kaulimbiu ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa kushirikiana ili kujenga jamii yenye usawa, ambapo kila mtu ana nafasi sawa ya kufanikiwa bila kujali jinsia yake.

     Katika dunia inayoendelea kubadilika, ni muhimu kuendelea kushinikiza sera na vitendo vinavyohakikisha wanawake wanapata haki zao kikamilifu.

    Siku hii hutumika kutoa wito wa kuchukuliwa  hatua kwa serikali, mashirika, na watu binafsi ili kuunda ulimwengu wenye fursa sawa kwa wote.

    11 min
  • Kenya : Mahakama ya madai madogo madogo

    Wakenya wameshauriwa kutochukua hatua mikononi iwapo wana mzozo wa malipo baina yao na watu wanaowadai.

     

    Hii ni baada ya maafisa wanahudumu mahakamani, mawakili na asasi za kijamii kufanya mkutano wa kueneza uwepo Wa mahakama hizo nchini Kenya huku wakiwahimiza raia kutumia korti hiyo ambayo inatatua kesi chini ya miezi miwili. 

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    10 min
  • Haki ya wanahabari kutumia teknolojia ya AI

    Katika  hii ya kidijitali na inayobadilika kwa kasi, teknolojia ya akili mnemba (AI) imekuwa sehemu muhimu ya sekta mbalimbali, ikiwemo uandishi wa habari.

    Katika mkutano wa "Ubunifu AI kwa Mustakabali Endelevu wa Vyombo vya Habari" ulioandaliwa na Tamasha la Vyombo vya Habari Afrika kwa kushirikiana na taasisi ya Baraza Media Lab, wadau wa sekta ya habari walijadili kwa kina athari za AI katika tasnia hiyo ya wanahabari .

     Mkutano huo ulilenga kuelewa jinsi AI inavyoweza kutumiwa kwa uwajibikaji ili kuimarisha kazi ya wanahabari.

    Matumizi ya akili mnemba katika uandishi wa habari yanaweza kuboresha utendaji kazi wa wanahabari kwa njia mbalimbali.

     Kwanza, AI inaweza kurahisisha utafiti na uchambuzi wa taarifa kwa kasi zaidi, hivyo kuokoa muda wa wanahabari.

     Kwa mfano, AI inaweza kusaidia katika uchanganuzi wa data kubwa, kugundua mwenendo wa habari, na kutengeneza muhtasari wa matukio kwa haraka.

    Pili, AI inatoa fursa ya kuboresha uthibitishaji wa habari kwa kusaidia wanahabari kugundua habari za uongo au zilizopotoshwa.

    Hii ni muhimu katika enzi ya sasa ambapo habari za kughushi zinaenea kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii.

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    11 min
  • Kenya haki raia mtoto wa kike kupata elimu

    Shiniko zaidi zinazidi kutolewa kwa mtoto wa kike kuendelea kuwepeza uwezo wa kujiendeleza kimasomo, licha ya kwamba wengi wao sasa wapo katika nafasi nzuri kimasomo ukilinganisha na awali.

    Katika makala haya Benson Wakoli, amezungumza na wanafunzi wa kike kufahamu lengo lao kujiendeleza kimasomo.

    10 min
  • Kenya : Vijana wa Kenya hawana ajira

    Nchini Kenya kwa mjibu taasisi ya twakwimu za serikali vijana millioni 3.5 hawana ajira, kumbuka idadi hii inawewa kuwa ya juu zaidi .

    Vigezo kadhaa vikihusishwa na ukosefu huo wa ajira, wakati huu serikali nayo ikisema ipo katika juhudi za kuhakikisha vijana wapata ajira.

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    10 min

About Jua Haki Zako

From the publisher's feed

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

More shows like Jua Haki Zako

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

1 Listeners