Jua Haki Zako

Jua Haki Zako

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Jua Haki Zako episodes

  • Maandiko matakatifu yapewe nafasi kusuluhisha mizozo

    Katika makala haya tunaangazia safari ndefu ya amani katika mataifa yanayopitia migogoro, Shabaha ikiwa ni Sudan Kusini na Somalia.

    Mataifa haya yamepitia miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mizozo ya kisiasa, na changamoto za kiusalama ambazo zimeathiri mamilioni ya raia wao.

     Lakini katikati ya changamoto hizo, mashirika mbalimbali ya kimataifa na ya kikanda yamekuwa mstari wa mbele kusukuma gurudumu la amani.

    Skiza makala haya kufahamu mengi.

    11 min
  • Mashambulizi kupitia mitandao ya kijamii

    Mitandao ya kijamii na teknolojia za kidijitali zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunawasiliana, tunajifunza, tunafanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kitaifa kupitia mitandao. Lakini pamoja na manufaa haya, kumekuwa pia na changamoto kubwa: mashambulizi ya maneno, udukuzi wa akaunti, na hata ulaghai wa kifedha.

    Skiza makala haya kufahamu mengi.

    10 min
  • Dunia: watoto wanazidi kutumika kama vijakazi

    Mwezi wa Juni ulishuhudia matukio mawili muhimu ya kimataifa yakiangazia haki na ustawi wa watoto.

    Mnamo tarehe 12 Juni, dunia iliadhimisha Siku ya kupinga Ajira ya Watoto, (World Day Against Child Labor) ikirejelea takwimu za kutisha kwamba watoto milioni 160 duniani kote bado wamenaswa katika ajira ya watoto - wengi wakifanya kazi chini ya mazingira hatarishi.

    Skiza makala haya kufahamu mengi.

    11 min
  • Kenya : Haki ya kumiliki ardhi ya jamii ya wafugaji

    Jamii za wafugaji nchini Kenya, bado zinapitia changamoto za kumiliki ardhi, jamii hizo ni kama vile,Turkana, Samburu, Rendille, Borana, Gabra na nyingine , zimeathiriwa kwa muda mrefu na unyang’anyi wa ardhi wakati wa ukoloni, ambao uliendelezwa hata baada ya uhuru .

    Licha ya kutambuliwa kwa haki za jamii katika Katiba ya 2010 na kupitishwa kwa Sheria ya Ardhi ya Jamii ya mwaka 2016, jamii hizi bado zinakumbwa na changamoto za ardhi,unyang’anyaji wa mashamba na ukosefu wa haki za  kisheria—hali inayotishia siyo tu maisha yao bali pia utamaduni.

    11 min
  • EAC : Uhuru na haki ya wanahabari kujiunga miungano

    Kataika makala haya  tunajadili umuhimu wa wanahabari kuelewa na kulinda haki zao, hasa kupitia vyama na miungano ya waandishi wa habari.

    Katika mazingira ambapo uhuru wa habari uko mashakani, na waandishi wengi wanakumbwa na changamoto kazini, je, kuna msaada wowote wa pamoja?

    Ni moja tu ya maswali tunayatarajia kuyajibu kwenye makala ya haya.

    Skiza makala haya kufahamu mengi

    10 min
  • EAC : Wakimbizi wazidi kukimbia makwao wakitafuta amani

    Maelfu ya watu kote barani Afrika wanalazimika kuyahama makazi yao—wengine kwa sababu ya vita, wengine kwa sababu ya mateso au hali ngumu ya maisha. 

     Wanakimbilia nchi jirani wakitafuta usalama, hifadhi, na matumaini ya kuanza upya, lakini safari ya kuwa mkimbizi si rahisi, ni safari ya maumivu, vizingiti, na kupoteza mengi.

    Katika makala haya tunajadili visingiti wanavyokumbana navyo watu wanaokimbia maakazi yao kutokana na vita. 

     Skiza makala haya kufahamu mengi.

    11 min
  • Kenya : Haki ya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa

    katika makala haya mskilizaji tunazAma kuangazia  uamuzi wa kihistoria uliofanywa hivi majuzi na Mahakama ya juu zaidi ya Kenya kuhusu haki za mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ya dini ya Kiislamu—hasa kuhusu haki ya kurithi mali ya baba yake.

    Uamuzi huu umetangazwa kuwa hatua muhimu katika mapambano ya kuhakikisha kila mtoto anaheshimiwa na kulindwa kikatiba bila kujali dini au mazingira ya kuzaliwa kwake.

    Kwa miongo mingi, baadhi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa, hasa katika jamii za Kiislamu, wamekuwa wakinyimwa haki ya kurithi mali ya baba zao moja kwa moja  kwa mujibu tamaduni ya dini hiyo.

     

    Kufamu mengi skiza makala haya.

    10 min
  • Maziwa Makuu : Haki ya afya ya akili

    Afya ya akili ni nguzo ya kila mmoja wetu ili kuafikia haki nyingine muhimu.

    Benson Wakoli alifanya mazungumzo na bi Ann Maria Qwicha, mwanahabari na mtetezi wa haki za binadamu hasa afya ya akili ili kufahamu mengi zaidi katika mapambano haya ya kuhakikisha afya ya akili inalindwa.

    11 min

About Jua Haki Zako

From the publisher's feed

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

More shows like Jua Haki Zako

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mjadala wa Wiki by RFI Kiswahili

Mjadala wa Wiki

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

1 Listeners