
Sign up to save your podcasts
Or


Kwa wiki za hivi karibuni zimekuwa za misukosuko nchini Kenya, mitaa ya jiji la Nairobi na miji mingine mikuu imekuwa ikifurika vijana… wakiwa na mabango mikononi, miili yao ikiwa tayari kwa chochote — hata kwa gesi ya kutoa machozi na risasi.
Lakini maandamano haya yanamaanisha nini? Vijana hawa wanadai nini? Na wanaruhusiwa kisheria kufanya hivyo? Ndio maswali tutakayokuwa tunayajibu kwenye makala haya.
Karibu katika makala ya Jua Haki Zako – makala ambayo siku zote hukuelemisha kuhusu haki zako tena za msingi jina langu ni benson Wakoli
Katika kila kona ya dunia, sauti za wanawake zimekuwa zikipigania jambo moja kuu – haki.
Haki ya kusikilizwa, Haki ya kuthaminiwa, Haki ya kupewa nafasi sawa. Na hapa Africa Mashariki ingawa hatua zimepigwa, safari ya mwanamke kuelekea usawa bado ina changamoto, katika hali ya vita kama vile, Mashariki mwa DRC, nchini Sudan Kusini na kaskazini, kaskazini mwa Ethiopia na pia Musumbiji.
Skiza makala haya kufahamu juhudi zinafanywa na shirika la Women For Women kutetea haki za wanawake kwenye maeneo ya vita, licha misaada kupunguzwa.
Katika makala haya tunajikita kuangazia hali ya haki ya wanawake Mashariki mwa DRC baada waasi wa M23 kufaulu kudhibiti miji ya Goma na Bukavu.
Tunazungumza na wakili Maggie Mkulima Shukru kutoka jijini Bukavu kutueleza hali ilivyo mashariki mwa DRC.
Skiza makala haya kufahamu mengi.
Kadri Afrika inavyozidi kuingia katika ulimwengu wa kidijitali, kila siku mamilioni ya watu wanaingia mitandaoni—kutafuta taarifa, kuwasiliana, kufanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kisiasa.
Lakini swali kuu ni Je, watu wote wanaelewa haki zao katika mazingira haya mapya ya kidijitali?
Skiza makala haya kufahamu mengi.
Kwenye makala haya tunaendeleza mahojiano yetu na Njeri mwangi mwanaharakati wa kutetea haki za kijisia Njeri mwangi
Skiza makala Kufahamu mengi
Nchini Kenya, harakati za kutetea njisia inazidi kushika moto mwanaharakati Njeri Mwangi, akiendelea kuhamasisha raia.
Skiza makala haya kufahamu mengi.
Shirika la Amnesty International imeitaka serikali ya Kenya pamoja na ile ya Saudi Arabia kushiriiana na kuweka mikakati ya kuhakikisha haki za raia wa Kenya wanaofanya kazi katika mataifa ya Ugaibini hazitatiziki.
Katika ripot iyake Amnesty imesema kuwa wanawake wanaofanya kazi za nyumbani huko Uarabuni wanapitia mateso za kijinsia, kunyanyashwa kimapato na hata kuuawa.
Katika makala haya tunazama kuangazia swala zima la demokrasia na uhusiano wake na haki za binadamu.
Unavyofahamu mskilizaji demokrasia mara nyingi hotofautiana na mazingira ya nchini mbalimbali duniani.
Mara kadhaa swala demokrasia limehusishwa na haki za binadamu, katika makala haya Benson Wakoli anajadili swala hili na muasisi wa shirika la utafito la Afro barometer Jane Wanga ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi kufahamu uhuasiano uliopo kati ta demokrasia na haki za binadamu.
Wafanyakazi ndio wanainua majengo, kufundisha watoto, kuwahudumia wagonjwa, kuendesha uchumi wa Afrika Mashariki.
Lakini je, haki za wafanyakazi kazini zinalindwa ? kila mwaka Mei mosi dunia huadimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi — na kwenye makala haya, tunaangazia kilio na matumaini ya wafanyakazi wa Afrika Mashariki wanaopigania haki zao za msingi kazini.
Muungano wa kimataifa wa wafanyakazi — ILO — linatambua haki kadhaa muhimu kwa kila mfanyakazi moja ni :
Haki ya kupata mshahara wa heshima
Haki ya kufanya kazi kwa saa zinazokubalika
Haki ya kujiunga na vyama
Haki ya usalama kazini
Haki ya kutobaguliwa
Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
Nchini Tanzania, wafuasi na wanasiasa wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, walikamatwa na kupigwa na maafisa wa polisi walipokwenda Mahakamani jijini Dar es salaam, kusikiliza kesi ya uhaini na uchochezi inayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani CHADEMA, Tundu Lissu.
Katika makala ya leo ya Jua Haki yao, tunaangazia Uhuru wa kufauta kesi mahakamani, kwanini kuna haki ya kusikiliza kesi mahakamani na kwa nini mataifa mengi barani afrika yanazuia raia kusikiliza kesi kama hizi mahakamani.
From the publisher's feed
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

2 Listeners

0 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

1 Listeners