
Sign up to save your podcasts
Or


Katika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na
desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali
inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa.
Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata
tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa
kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu
na kupiga marufuku tendo hilo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa
ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15
hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya.
Katika makala haya tunaangazia namna tamaduni
hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama
hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata
elimu na kuishi bila unyanyasaji.
Katika makala haya tunangazia safari ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia hadithi sauti moja, uzoefu, na ujasiri wa mtu kusimulia alichopitia.
Tasisi ya Moth, imekuwa ikitumia hadithi kama si tu kwa mudhadha wa burudunai bali ni daraja linalounganisha ukweli wa mtu mmoja na uelewa wa dunia nzima.
Hadithi nyingi ni za binafsi, lakini hisia zinazozibeba—hofu, matumaini, maumivu au ushindi—ni za ulimwengu mzima.
Skiza makala haya kufahamu mengi.
Mila na tamaduni kutoka jamii mbalimbali nchini Kenya, zimezidi kukandamiza wanawake kutoridhi mali.
Pwani ya Kenya, changamoto hiyo pia imeathiri wanawake wajane skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
Katika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC hasa eneo la Mashariki, ambapo tunajadili haki za malemavu eneo hilo.
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamia ya watu wenye ulemavu wamejikuta wakihangaika kuokoa maisha yao, kipindi hiki vita vikiendelea kusheheni eneo hilo.
Miji kama Goma, Rutshuru na Sake imeshuhudia maelfu wakikimbia maakazi yao. Lakini kwa wengi wenye ulemavu, kukimbia si jambo rahisi.
Wengine wanatembea kwa magongo, wengine hutumia viti vya magurudumu ambavyo haviwezi kuvuka matope, milima, au mabonde.
Skiza makala haya kufahamu mengi
Uchaguzi nchini Uganda, unatarajiwa kufanyika mwezi January, Rais Museveni akichuana tena na Hasimu wake wa kisiasa mwanamziki aliyeukia siasa, Bobi Wine.
Skiza makala haya kufahamu mengi.
Katika makala haya tunaangazia suala linalozidi kuwa pasua kichwa—unyanyasaji wa wanawake kwenye mitandao ya kijamii.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirikisho la mawakili wanawake nchini Kenya FIDA, kwa ushirkiano na wenzao wa kutoka nchini Nigeria, unaonesha kuwa karibu kila mwanamke anayetumia mitandao amewahi kushambuliwa iwe ni kwa maneno ya matusi, vitisho, au kusambaziwa picha binafsi bila idhini yake.
Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
Watoto wanatumika kwa baishara ya ngono
Skiza makala haya kufahamu mingi zaidi
Katika makala haya tunaangazia hatua ya kihistoria kwa jamii ya wafugaji nchini Kenya.
Jamii ya Wayu Daba imekabidhiwa rasmi hati miliki ya ardhi yao kupitia Mpango wa Kusimamia Ardhi Kidigitali, unaoendeshwa na serikali mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO.
Hati hii inaguza maeneo makubwa ya ardhi, ikiwemo ardhi loevu yenye rutuba, misitu ya kiasili yenye wanyama na mimea adimu, pamoja na maliasili zinginezo ambazo zimekuwa nguzo ya maisha ya jamii hiyo kwa vizazi vingi
Skiza makala haya kufahamu mengi.
Katika makala haya tutajadili haki za mwandishi wa vitabu, Je, mwandishi wa kitabu ana haki gani anapochapisha kitabu chake katika mashirika ya uchapishaji? Ni kipi kinafaa kuzingatiwa katika mchakato wa uchapishaji?
Maswali haya yote yanamzunguka mwandishi, mchapishaji na shirika la uchapishaji ili kuibuka na mwafaka katika tasnia ya uandishi.
Na ndiyo baadhi ya mambo yanayojadiliwa kwenye makala haya.
From the publisher's feed
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

2 Listeners

0 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

1 Listeners